banner

July 10, 2016

SIMBA YAYUMBA KIUNGO , MKUDE ATIMKIA AFRIKA KUSINI MAJABVI HARUDI

SIMBA YAYUMBA KIUNGO , MKUDE ATIMKIA AFRIKA KUSINI MAJABVI HARUDI

Wakati Yanga na Azam wakijazia mapengo katika vikosi vyao vilivyomaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili msimu uliopita, kazi ya kuijenga upya Simba imezidi kuwa kubwa kufuatia dalili za kuwakosa viungo wake tegemeo kudhihirika.

Viungo wakabaji, Jonas Mkude na Justice Majabvi wana kila dalili za kutokuwemo katika kikosi cha Simba msimu ujao.

Mkude yupo nchini Afrika Kusini kwa majaribio katika moja ya klabu ya ligi kuu nchini humo. Kiungo huyo aliondoka nchini wiki iliyopita kujaribu bahati yake kwa mara ya pili baada ya awali kufanya hivyo na kukosa nafasi katika klabu ya Bidvest Wits.

Majabvi, raia wa Zimbabwe ambaye alikuwa moja ya nguzo muhimo katika kuikinga safu ya ulinzi  msimu uliopita yupo katika mipango ya kuhamia nchini Austria alikowahi kucheza soka la kulipwa.

kikosi cha Simba kimeagwa hii leo na mashabiki, viongozi na wanachama tayari kuelekea mkoani Morogoro kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu.


Bofya HAPA Ku-install App ya Ruwehy Official ili usi sumbuke kuingia kwenye website

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search