banner

July 01, 2016

WATU WASIJULIKANA WAFANYA UHARIBIFU WA MIGOMBA NA MIFUGO PEMBA

WATU WASIJULIKANA WAFANYA UHARIBIFU WA MIGOMBA NA MIFUGO PEMBA

Kwa mara nyengine tena watu wasio julikana wamefanya hujuma ya kuharibu migomba na kunyonga mifugo ya muakilishi mstafu wa kuteuliwa na rais Hasnuu Muhamed Haji huko Chogooni Mgelema katika wilaya Chakechake. 
Watu hao waliofika katika shamba hilo walifyeka migomba wakawakata vichwa kuku na kutoroka na Mbuzi walio kuwemo kwenye banda.
  
Akizumza mara baada ya kuangalia tukio hilo mkuu wa mkoa Kusini Bimwana Juma Majidi Abdalla amewaasa wananchi wanaondelea kufanya vitendo vya uhalifu na uhujumu wa mazao kwa kushawishiwa kuacha kufanya vitendo hivyo kwani havitawasaidia wao na hao wanaowatuma.
Akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na kushamiri kwa matukio hayo naibu mkurugenzi wa makosa jinai Zanzibar naibu kamishina Salumu Msangi ametoa onyo kwa wanaojihusisha au kuhamasisha wananchi kuendelea kufanya vitendo vya hujuma kwa wananchi.
Kamanda Msangi alisema tayari wamekwisha kamata watu kadhaa na kwamba Jeshi la polisi linawasaka watuhumiwa wengine akiwemo mkurugenzi wa mipango na uchauguzi wa CUF na mwakilishi mstafu wa jimbo la Chakechake chama cha wananchi CUF Omar Ali Shehe na kumtaka ajisalimishe. 
Miongoni mwa Kuku ambao ni mali ya Hasnuu Moh'd Hassan, walionyongwa na watu wasiojuilikana huko katika Bonde la Chogooni , Chonga Pemba.
 Baadhi ya Migomba ya Hasnuu Moh'd Hassan, ambayo imekatwa na Watu wasiojulikana huko katika Bonde la Chogooni -Chonga Pemba.
 Hasnuu Moh'd Hassan wa Chonga Wilaya ya Chake Chake Pemba, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya kufanyiwa hujuma za mali zake.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya hujuma zinazofanywa na watu wasiojulikana kwa wananchi wenzao .

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search