banner

December 28, 2016

STEREO ASHINDWA KUZUIA HISIA ZAKE ZA NDANI KWA RAPA CHEMICAL, AFUNGUKA HAYA

STEREO ASHINDWA KUZUIA HISIA ZAKE ZA NDANI KWA RAPA CHEMICAL, AFUNGUKA HAYA

Rapa Stereo amefunguka ya moyoni na kuweka hisia zake za ndani juu ya Rapa Chemical na kusema kuwa anampenda kwa dhati na anahitaji kuwa naye kama mpenzi wake.

Stereo alieleza hisia zake juu ya Chemical na kusema ni muda mrefu amekuwa akimpenda na hakuwahi kumwambia ukweli huo kwa kuwa hakuwahi kupata nafasi ya kuonana naye na kuongea naye.
Stereo anasema ameona itakuwa si vyema ukaisha mwaka 2016 bila kuliweka wazi jambo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu moyoni kwake
“Kiukweli nampenda sana Chemical kutoka moyoni, namzimia muda mrefu hata washikaji zangu wa karibu wanalitambua hilo nasema haya maneno dunia yote ijue kuwa namzimia Chemical, nazungumza maneno haya nikiwa na akili timamu sijalazimishwa na mtu ila ni ukweli uliopo moyoni mwangu” alisema Stereo kwenye Planet Bongo.
Kwa upande wake Chemical baada ya kumsikia Stereo Redioni alisema ni wazi inaonyesha anachokisema Stereo kinatoka moyoni ila kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kwani
yeye anampenda Stereo kama kaka yake, na pia anaamini mapenzi ni hisia zaidi, kwa kuwa hajapata nafasi ya kukaa naye na kuongea naye hawezi kujua nini kitaendelea.
“Kiukweli nimekuwa suprised sana kumsikia stereo sikutegemea kumsikia akizungumza maneno hayo ila anavyozungumza alikuwa akiongea kwa hisia inaonyesha jambo hilo linatoka moyoni mwake” alisema Chemical

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search