banner

January 02, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA KABYAILE MISENYI MKOANI KAGERA

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA KABYAILE MISENYI MKOANI KAGERA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiwa wameshika utepe huo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

Taaswira ya moja ya jengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumapili Januari Mosi, 2017 ameendelea na ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha Kabyaile kilichopo Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera 

Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo hicho cha Afya Rais Dkt Magufuli amesema serikali kwa sasa imeweka nguvu kubwa katika kurejesha miundo mbinu ya huduma za jamii iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10,2016 Mkoani humo badala ya kujenga nyumba ya mwananchi mmoja mmoja. 

”Na ndio maana nimeona leo hapa tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2017 niwaeleze ukweli maana kuna watu wanapitapita huko na wapo wengine nyumba zao zilibomoka kidogo wakadanganywa wakaambiwa kuwa serikali itakuja kuwajengea nyumba wakazibomoa zote ”waafwa” kama ulitegemea ukiibomoa utalipwa fidia,hakuna” 

Aidha Dkt Magufuli amemwagiza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kupeleka huduma ya umeme katika kituo hicho cha afya alichokiwekea jiwe la msingi,ambapo pia ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Bilioni moja kwa ajili kutengeneza barabara inayoelekea kituoni hapo kwa kiwango cha lami. 

Pia ameuagiza uongozi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaojenga kituo hicho cha afya kuharakisha ujenzi wake na kukamilika kabla ya mwezi februari badala ya Machi mwaka huu. 

Dkt Magufuli ameutaka uongozi na wananchi wa Wilaya ya Misenyi na maeneo mengine nchini kutumia vyema mvua chache zinazonyesha mkoani humo kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ili kuepukana na baa la njaa na kwamba serikali haina mpango wa kugawa chakula cha bure. 

Jaffar Haniu 
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Kagera. 
01 Januari, 2017
 
ILI KUSOMA HABARI ZA UHAKIKA KILA SIKU DOWNLOAD APP YETU YA ZOTE KALI BLOG KWENYE SIMU YAKO BONYEZA HAPA NI BUREE

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search