banner

February 23, 2017

CRISTIANO RONALDO ASHINDWA KUISAIDIA REAL MADRID KUZAMA

CRISTIANO RONALDO ASHINDWA KUISAIDIA REAL MADRID KUZAMA

Vinara Real Madrid wamepata kipigo cha pili katika Ligi ya La Liga katika msimu huu baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Valencia.

Mshambuliaji wa zamani wa West Ham, Simone Zaza alikuwa wa kwanza kufunga goli kwa wenyeji na kisha Fabian Orellana kuongeza goli la pili kabla ya Cristiano Ronaldo kuchomoa moja.

Cristiano Ronaldo ambaye aliondoa gundu la kutofunga kwa muda alikosa nafasi ya kuisaidia Real Madrid kuambulia pointi moja baada ya mpira wake wa kichwa ulikosa kulenga goli.
                                    Cristiano Ronaldo akikimbia na mpira baada ya kufunga goli
                                       Gareth Bale akiwa ameshika kiuno baada ya jahazi kuzama

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search