banner

February 22, 2017

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA JACKSON MAYANJA KUJIHAKIKISHIA USHINDI DHIDI YA YANGA FEB 25

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA JACKSON MAYANJA KUJIHAKIKISHIA USHINDI DHIDI YA YANGA FEB 25


Kuelekea Mechi ya Simba na Yanga Feb 25 Mayanja amesema, mchezo wao dhidi ya Yanga ni wa kufa na kupona huku akisisitiza Simba imejipanga kupata ushindi moja kwa moja

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema, hawataki kufikia sehemu kuanza kupiga hesabu na wapinzani wao Yanga kuhusu nani atatwaa ubingwa wa msimu huu, wanachotaka wao ni kushinda mechi ya Jumamosi Februari 25 ili kuwaacha Yanga kwa pointi nyingi kuliko kusubiri hesabu ziamue nani anakuwa bingwa.


Mayanja amesema, mchezo wao dhidi ya Yanga ni wa kufa na kupona huku akisisitiza Simba imejipanga kupata ushindi moja kwa moja.
“Kwetu hiyo ni mechi ya kufa na kupona, tumejiandaa vizuri sitaki kudanganya mtu. Ushindi utatupa nafasi nzuri ya kushinda ubingwa lakini kama tutashindwa kwenye mechi hiyo tutaenda kwa hesabu sasa sisi hatutaki kufikia huko, hii ni mechi ya ushindi moja kwa moja,” – Jackson Mayanja aliwaambia waandishi.

 “Mazoezi yanaendelea vizuri sana, tunataka kuona tunacheza mechi hiyo kwa kiasi kikubwa hiyo ndio mechi ya mbio za ubingwa kati ya Simba na Yanga na endapo tutashinda tutakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuwa mabingwa wa mwaka huu.”
Mayanja alipoulizwa kuhusu maendeleo ya beki wo wa kati Method Mwanjali alisema hayupo tayari kuzungumzia mchezaji mmoja.


“Wachezaji wa timu zote wanaweza kupata majeruhi, lakini Simba haitegemei mchezaji mmoja na mpira wa Simba msimuu ni wa kitimu lakini kama kuna majeruhi bado ni mchezaji wa simba kama anakuwa vizuri tunamuhitaji kama hajawa vizuri tunamwacha aendelee kupumzika.”


Mwanjale hakumaliza mazoezi yote ya jana, alifanya kwa muda mfupi kisha akapumzika. Beki huyo ambaye kwa sasa ndio tumaini la Simba kwenye idara ya ulinzi aliumia kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Prisons na kushindwa kuendelea na mchezo.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search