banner

February 25, 2017

MASHABIKI SIMBA, YANGA WAPEWA ONYO

MASHABIKI SIMBA, YANGA WAPEWA ONYO

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeonya mashabiki wa soka nchini kuacha kuingiza siasa kwenye mpira na kwamba atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua.
Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema jana Dar es Salaam kuwa, amepata taarifa juu ya mashabiki wamepanga kwenda kuchana kadi za vyama vya siasa uwanjani, jambo ambalo ameonya kwa atakayefanya hivyo sheria itachukua mkondo wake.
Alisema uwanjani sio sehemu ya siasa bali mpira hivyo, watu waende kuhamasisha timu.
“Tumesikia kuna watu wanataka kwenda uwanjani na kadi za vyama vyao kwenda kuchana, sasa kule sio mahali pake na kwa atakayethubutu kufanya hivyo, basi watu wa usalama wako pale,”alisema.
Lucas alisema watu hao ambao hakuwataja majina walipanga kwenda kwenye mechi ya Simba na Yanga na kadi za vyama vya siasa, kuhamasisha siasa zao.
Hilo ni onyo la pili baada ya hivi karibuni kudaiwa kuna mashabiki walipanga kwenda kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Ngaya ya Comoro na mabango ya kutuhumu serikali na baadhi ya viongozi.
Hata hivyo, katika mechi ya Yanga dhidi ya Ngaya ambayo ndio hasa mashabiki hao walitaka kutumia mabango yenye ujumbe mzito kwa viongozi wa serikali hayakuwepo baada ya kutii onyo la TFF.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search