banner

February 25, 2017

NMB YASAIDIA KOMPYUTA 50 SHULE Z’BAR

NMB YASAIDIA KOMPYUTA 50 SHULE Z’BAR

BENKI ya makabwela (NMB) imetoa msaada wa kompyuta 50 kwa shule za msingi na sekondari za visiwani Zanzibar.
Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi wa NMB, Ineke Bussemaker kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma, aliyesema unalenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha elimu.
Bussemaker alisema NMB inaunga mkono juhudi za Serikali za kukuza kiwango cha elimu nchini, hususan katika masomo ya Tehama.
Alisema msaada huo utazinufaisha shule za msingi na sekondari tisa pamoja na chuo cha ualimu kimoja kitakachopatiwa kompyuta mpakato tano.
“Kompyuta hizo ni sehemu ya kompyuta zaidi ya 250 ambazo tayari zimeshakabidhiwa Tanzania Bara kwa ajili ya shule za msingi na sekondari.
Kompyuta hizo zilishatumika na benki ya NMB kwa miaka mitatu, huku zikiwa bado kwenye hali nzuri kwa ajili ya matumizi.
 “Tumetoa msaada wa kompyuta 50 zilizokwishatumika miaka mitatu kwa ajili ya shule za msingi na sekodari, zipo katika hali nzuri kwa matumizi ya wanafunzi na wataalamu wetu wa ICT wamethibitisha na tunaamini zitatumika vizuri na kuwa na faida katika masomo ya Tehama,” alisema Bussemaker.
Akipokea kompyuta hizo, Waziri Juma alisema msaada huo umetolewa wakati muafaka  kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search