Matokeo hayo yanaifanya Genk isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya wiki iliyopita kulazimisha sare ya 2-2 ugenini.
Bao la Genk katika mchezo wa jana uliochezeshwa na refa Mholanzi, Serdar Gozubuyuk lilifungwa na kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 67.
Mbwana Samatta (kushoto) akimpongeza Alejandro Pozuelo baada ya kufunga bao pekee jana |
Ratiba ya 16 Bora itapangwa leo mchana na mechi za kwanza zitachewa Machi 9 na marudiano yatakuwa Machi 16, mwaka huu.
Aidha, jana Samatta jana amecheza mechi yake ya 44 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 26 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 25 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 14 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Ryan, Castagne, Colley, Brabec, Uronen, Berge, Malinovskyi/Boetius dk90, Pozuelo/Kumordzi dk89, Trossard, Authors/Buffalo dk76 na Samatta.
FC Astra Giurgiu : Lung, Morais Alves, Săpunaru, Stan Seto/Ionita dk82 Mansaly, Lovin/Bus dk70 Budescu, Niculae/Florea dk67 na Teixeira.