banner

March 12, 2017

MAGOLI YA DAVID SILVA NA SERGIO AGUERO YAIPATIA USHINDI MANCHESTER CITY

MAGOLI YA DAVID SILVA NA SERGIO AGUERO YAIPATIA USHINDI MANCHESTER CITY

Magoli kutoka kwa David Silva na Sergio Aguero na kuipatia Manchester City ushindi waliostahili dhidi ya Middlesbrough na kutinga nusu fainali ya FA.

Silva alifunga ndani ya dakika tatu katika umbali wa yadi 6 baada ya Pablo Zabaleta kupata muda na nafasi ya kutoa krosi iliyozaa goli.

Kipa wa Middlesbrough, Brad Guzan, aliokoa michomo mikali ya Silva, Leroy Sane na mpira uliobadili mwelekeo wa shuti la Aguero.

Hata hivyo Aguero hatimaye alifanikiwa kuwatungua wageni alipounganisha krosi ya Sane na kujihakikishia kucheza nusu fainali Wembley.

  Sergio Aguero akiangalia mpira uliopigwa na Silva ukijaa wavuni na kumshinda kipa Guzan

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search