banner

March 29, 2017

MWANJALI ATIA NENO KAGERA SUGAR VS SIMBA SC

MWANJALI ATIA NENO KAGERA SUGAR VS SIMBA SC

Beki wa kati wa Simba SC, Mzimbabwe Method Mwanjali amewataka wachezaji wenzake wa klabu hiyo kujibidiisha kushinda kila mechi ili watimize ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
“Mimi bado ninaumwa, lakini napenda kuwatakia kila heri wachezaji wenzangu waisaidie timu kushinda. Wajitume washinde kila mechi ili tuchukue ubingwa,”alisema Mwanjali Dar e Salaam jana mchana.
Mwanjali hajaenda Bukoba kwa sababu anauguza goti aliloumia katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Prisons Februari 11, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ikishinda 3-0.
Siku hiyo, Mwanjali aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC, alitolewa kwa machela siku hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Mwinyi Kazimoto dakika ya 62.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search