banner

March 29, 2017

TIRA YAJIDHATITI KURUDISHA THAMANI YA BIMA

TIRA YAJIDHATITI KURUDISHA THAMANI YA BIMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imejizatiti kurudisha thamani ya huduma za bima kwa kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni za bima  pamoja na kutengeneza mfumo wenye kutoa  tija kwa Wananchi, Serikali pamoja na Kampuni za Bima nchini.
Hayo yamesemwa mapema hii leo Jijini Dar es salaam na Kamishna wa Bima, Baghayo Saqware alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya namna mamlaka hiyo ilivyojipanga kurudisha thamani ya bima kwa wananchi na makampuni ya bima hapa nchini.
Saqware amesema kuwa moja ya kanuni na sheria zitakazoboreshwa ni pamoja na kupeleka biashara ya bima (Insurance business – risks) nje ya nchi badala ya kutumia makampuni ya ndani.
“Tutaweka kanuni itakayolazimisha Kampuni za bima hapa nchini kuongeza mitaji au kutengeneza mfuko wa pamoja au mfumo wa makampuni kushirikina kimtaji ili kuweza kuandikisha na kubakisha sehemu kubwa au biashara yote ya bima nchini,” amesema Saqware.
Aidha, amesema kuwa ikibidi mamlaka hiyo itabadilisha sheria ya bima nchini ili wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi (import goods) iwe ni lazima kukatia bima nchini  ili kuongeza mapato ya kodi (VAT) pamoja na bima (Premium Levy).
Katika kurudisha thamani ya huduma ya bima kwa wananchi mamlaka hiyo itahakikisha makampuni yanayotoa huduma ya bima yanatoa huduma stahiki kwa wateja wa bima pamoja na kuhakikish malalamiko ya wateja yanayofikishwa  katika mamlaka husika yanashughulikiwa kwa wakati.
Nae, Meneja Tehama TIRA, Aron Mlaki amesema kuwa mfumo huo wa Tehama utamuwezesha mwananchi kupata maelezo ya  bima yake kupitia intanenti na meseji za kawaida ambapo kwa upande wa message za kawaida ataandika  neno ‘STIKA’ likifuatiwa na namba ya Stika na kuituma kwenye namba 15200 baada ya hapo atapokea taarifa za bima yake.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search