Tangaza nasi

April 20, 2017

STORI KUBWA : Hazard Huyoo Madrid, Soma Taarifa za Usajili Barani Ulaya

Real Madrid imefikia makubaliano na winga wa Chelsea Eden Hazard ya kujiunga na klabu hiyo kwenye dirisha la usajili la mwezi Juni.
Daily Star linaarifu kuwa kiungo huyo mshambuliaji ameonyesha nia ya kuichezea Madrid huku akisema kocha Zinedine Zidane alikuwa ni mmoja wa wachezaji aliokuwa akiwakubali sana huku Mfaransa huyo pia akimwagia sifa nyingi Hazard kila mara.
Siku chache zijazo Madrid itaingia katika mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa mshambuliaji huyo huku wachezaji kama James Rodriguez na Alvaro Morata wakijumuishwa katika dili hilo.
PSG NAO WAJITOSA KWA OZIL
Kiungo Mesut Ozil ameendelea kuhusishwa na kutaka kuondoka Arsenal na sasa klabu ya matajiri wa Ufaransa Paris St Germain wakiingia katika kinyang’anyiro hicho cha kupata saini yake
PSG ambao wanamtaka Alexis Sanchez pia huenda wakaanza na usajili wa Ozil kwani wamemuweka namba moja katika orodha yao. Ozil amebakiza miezi 15 katika mkataba wake na Arsenal
Uchumi wa klabu ya PSG huenda ukaisaidia klabu hiyo kuzipiku Manchester United, Bayern Munich na Chelsea ambazo zimeonesha nia ya kumnasa Mjerumani huyo.
UNITED, SPURS WAMGOMBANIA MERTENS
Mshambuliaji wa S.S.C Napoli Dries Mertens amezingiiza vitani klabu za Manchester United na Tottenham Hotspurs juu ya saini yake kutokana na kiwango bora alichokionyesha msimu huu.
Mertens amepachika mabao 21 katika michezo 29 yakiwemo mabao matano katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kutakuwa na ugumu kumnyakua mshambuliaji huyo kwani DH inaarifu kuwa atapewa mkataba na mshahara aliokuwa akiutaka na hivyo kufanya uhamisho wake kwenda klabu nyingine kuwa mgumu.
LIVERPOOL YAKARIBIA KUMNASA HART
Mlinda mlango wa Manchester City aliyepo kwa mkopo katika klabu ya Torino nchini Italia Joe Hart huenda akajiunga na majogoo wa Anfield Liverpool baada ya klabu hiyo kuwa tayari kumsajili.
Golikipa huyo amekuwa katika tetesi zikimuhusisha na klabu mbalimbali barani Ulaya zikiwemo West Ham United na Arsenal ila Liverpool imeonyesha nia ya dhati ya kumnasa katika majira ya joto.
Liverpool ipo tayari kutoa kitita cha paundi 20 milioni ambacho Man City wanahitaji ili kumwachia Muingereza huyo.
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka