banner

April 28, 2017

STORI KUBWA NA TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO APRIL 28 : Hapa Ronaldo Pale Mbappe Madrid

STORI KUBWA NA TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO APRIL 28 : Hapa Ronaldo Pale Mbappe Madrid

Kinda wa AS Monaco Kylian Mbappe ambaye yupo kwenye kiwango bora kwa sasa huenda akajiunga na Real Madrid baada ya miamba hiyo ya Hispania kumuandalia dau mwezi Juni.
Huenda ndoto yake ya kucheza na nyota Cristiano Ronaldo ikakamilika karibuni baada ya Madrid kumuandalia dau la euro 100 milioni kufuatia kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane kupendekeza dili hilo.
Mbappe amekua akiota kucheza na Ronaldo tangu mdogo na akiwa na picha za nyota huyo katika chumba chake ikiwa ishara ya kuonyesha jinsi gani anamkubali.
MESSI, INIESTA KUBAKI BARCA

Nahodha Andres Iniesta na nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi wanategemewa kusaini mikataba mipya hivi karibuni kwa mujibu wa katibu mwenezi Robert Fernandez.
“Iniesta na Messi watasaini hivi karibuni. Iniesta amesema kuwa atasubiri hadi mwisho wa msimu. Klabu itaamua lini itangaze mkataba wa Messi na makubaliano ya muda wake,” alisema katibu huyo.
Kumekuwa na taarifa juu ya klabu hiyo kutafuta mbadala wa Iniesta kutokana na umri wake kuzidi kusogea na ufanisi kupungua.
SANCHEZ KUUZWA NJE YA UINGEREZA

Kocha wa Arsensl, Arsene Wenger ameahidi kutomuuza mshambuliaji wake nyota Alexis Sanchez kwa timu pinzani za ligi kuu nchini Uingereza kufuatia mchezaji huyo kukaribia ukingoni mwa mkataba wake.
“Nilimuachia Van Persie kwasababu alikuwa na umri wa miaka 29 akielekea 30 na alikuwa anasaini mkataba mrefu hilo ni tofauti kwa Sanchez, asiposaini tutamfanya abakie na sintomuuza kwa wapinzani ni bora abakie hapa,” alisema Wenger.
Klabu pinzani zinazoshiriki ligi kuu nchini Uingereza za Chelsea, Manchester City na Manchester United zimeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo raia wa Chile aliyebakiza miezi 15 katika mkataba wake.
BENCHI KUMRUDISHA BELLERIN BARCELONA

Kufuatia kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kubadili mfumo wa uchezaji na upangaji timu, beki wa kulia Hector Bellerin ameanza kuwaza kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Taarifa kutoka Diario Gol inasema wawakilishi wa klabu ya Barcelona wamewasili katika jiji la London kufatilia uwezekano wa kumnyakua beki huyo.
Wawakilishi hao huenda wakafanikiwa na kurudi Hispania wakiwa na furaha kwani Kitendo cha Wenger kutumia mfumo wa 3-4-3 kimemfanya beki huyo kukosa nafasi katika kikosi hicho cha kwanza.
ARGENTINA KUMPA KIBARUA SAMPAOLI

Chama cha soka nchini Argentina (AFA) kimethibitisha kumpa ofa kocha wa Sevilla Jorge Sampaoli ili kuitumikia timu ya utaifa wake.
“Naweza kuthibitisha kuwa ni chaguo pekee tulilonalo na tunawaheshimu Sevilla sababu bado anafanya kazi huko.Sasa Tutaingia dili la kumtoa Sevilla na kuna kipengele itabidi tukizungumzie,” Tapia aliiambia ESPN.
Sampaoli alitua Sevilla kuchukua mikoba ya Unai Emery aliyetimkia Ufaransa. Muargentina huyo amefanya kazi kubwa kwa muda mfupi kuiimarisha Sevilla na kuiweka katika nafasi ya kushiriki klabu bingwa barani Ulaya.
ANCELOTTI YUPO SALAMA LICHA YA VIPIGO

Kufuatia vichapo vya hivi karibuni ilivyopokea Bayern Munich ikiwa imeshindwa kushinda katika michezo mitano iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Karl Heinz Rumminegge amemtoa hofu kocha Carlo Ancelotti.
“Carlo Ancelotti ni Kocha mzuri na mzoefu, mkataba wake unajulikana unaisha 2019 na hilo halina mjadala,” alisema Rumminegge.
Bayern imejikuta ikitolewa katika michuano ya kombe la ligi na Borussia Dortmund na klabu bingwa barani Ulaya hatua ya Robo Fainali na Real Madrid na kuiacha klabu ikiwa inajiuliza juu ya uwezo wa kocha huyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search