banner

May 04, 2017

AZAM WAPANIA KUIKALISHA MBAO

AZAM WAPANIA KUIKALISHA MBAO

NA TIMA SIKILO,
AZAM wamesema watahakikisha wanaikalisha Mbao FC katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, meneja wa timu hiyo, Philipo Alando, alisema wanaendelea na mazoezi makali ili kuwajengea ufiti wachezaji wao.
Alando alisema malengo yao ni kuibuka na ushindi na kujiongezea pointi ili waweze kumaliza katika nafasi bora kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Alisema wachezaji wao wana ari kubwa ya kuondoka na ushindi kutokana na mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Alando alisema watahakikisha wanawadhibiti wapinzani ambao wiki iliyopita waliifunga bao 1-0 Yanga katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Alisema kutokana na umuhimu wa mechi hiyo hawatakubali kupoteza katika uwanja wao wa nyumbani, kwani wamejipanga kuhakikisha wanabakisha pointi tatu.
Meneja huyo alisema kwa sasa hakuna majeruhi katika kikosi chake, lakini hawana pengo la Himid Mao aliyekwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa nchini Denmark.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search