banner

May 25, 2017

GRIEZMAN BADO YUPOYUPO ASEMA RAISI WA ATLETICO

GRIEZMAN BADO YUPOYUPO ASEMA RAISI WA ATLETICO

Madrid, Hispania. Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amesema mchezaji wake, Antonie Griezmann ataendelea kubaki kikosini hapo licha ya kuwepo taarifa kwamba ana nafasi kubwa ya kujiunga na Manchester United.
Rais huyo alisema kwa klabu yoyote yenye nia ya kumchukua nyota huyo ijiandae kuweka mezani Pauni 100 milioni. Griezmann amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye dimba la Old Trafford.
Licha ya kuendelea majadiliano hayo, mchezaji huyo hajazungumza chochote kuhusu uhamisho wake.
Mchezaji huyo mwenye miaka 26 ameiwezesha klabu hiyo kumaliza msimu huu katika nafasi ya 3, huku wakifuzu kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Rais huyo, alisema licha ya kuwapo tetesi hizo hakuna klabu ambayo imeshafika na kufanya naye mazungumzo rasmi. Hivyo wanachopaswa kutambua mchezaji huyo ana mkataba mpaka Juni mwaka 2021.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search