banner

May 29, 2017

HII HAPA RATIBA KAMILI YA SPORTPESA SUPER CUP 2017

HII HAPA RATIBA KAMILI YA SPORTPESA SUPER CUP 2017

Mwendelezo wa mapinduzi ya soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla umeshaanza chini ya Kampuni ya SportPesa, ambapo kwa sasa kinachosubiriwa ni michuano ya SportPesa Super Cup.
Michuano hiyo mifupi ambayo itashirikisha timu nne za Tanzania na Kenya inatarajiwa kuanza wiki ijayo.

Ikumbukwe kuwa Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alisema michuano hiyo mifupi inatarajiwa kuanza  Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11. 

Pia bingwa wa SportPesa Super Cup atabeba dola 30,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 66 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 22.

Mipango ya kuelekea kwenye michuano hiyo imeshaanza kwa upande wa timu zote zikiwemo Simba na Yanga ambazo ni klabu kubwa nchini Tanzania.

Huu ni mchangano wa ratiba ya michuano hiyo katika picha: 

RATIBA KAMILI YA SPORTPESA SUPER CUP 2017
Timu za Tanzania.
1. Simba.
2. Yanga
3. Singida United Fc
5. Jang'ombe Boys (Zanzibar)

Timu za Kenya
1. Gol Mahia
2. Tusker FC
3. FC Leopards
4. Nakulu

Juni 5, 2017 
AFC Leopards Vs Singida United
Saa 8:00 Mchana.

Yanga Vs Tusker
Saa 10:00 Jioni

Juni 6, 2017
Simba Vs Nakulu
Saa 8:00 Mchana

Gol Mahia Vs Jang'ombe
Saa 10:00 Jioni

UWANJA WA UHURU, DAR ES SALAAM

Nusu fainali
Juni 8, 2017 
Mshindi wa Singida United vs AFC Leopards atacheza na mshindi wa Yanga Vs Tusker.

Nusu fainali ya pili mshindi wa mechi Simba VS Nakuru All Stars atacheza na Jangombe Boys Vs Gor Mahia.

Fainali
Juni 11

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search