banner

May 24, 2017

IBRAHIMOVIC, SIR ALEX FERGUSON WAIBUKA MAZOEZI YA MANCHESTER UNITED

IBRAHIMOVIC, SIR ALEX FERGUSON WAIBUKA MAZOEZI YA MANCHESTER UNITED

Katika kile kinachoonekana kama fainali ya Europa League ni kubwa kwa Klabu ya Manchester United, wakongwe wa klabu hiyo wametua kwenye mazoezi kuongeza hamasa.
Kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson amewafanyia wachezaji wa timu hiyo ‘surprise’ kwa kufika mazoezini hapo siku moja kabla ya kusafiri kuelekea Sweden kucheza fainali hiyo dhidi ya Ajax.

Lakini wakati maandalizi ya kuelekea Stockholm yakifanyika, ghafla straika mkongwe wa timu hiyo, Zlatan Ibrahimovic naye aliwasili akiwa anaendesha kwenye gari, ambapo alikuwa amekaa siti ya nyuma.

Zlatan ambaye ana umri wa miaka 35 yupo nje akiuguza maumivu ya goti tangu alipoumia katika mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht, Aprili 20, mwaka huu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search