banner

May 24, 2017

KAMATI YA UTENDAJI YATOA TAMKO KWA MARA YA KWANZA KUHUSU MANJI KUJIUZULU

KAMATI YA UTENDAJI YATOA TAMKO KWA MARA YA KWANZA KUHUSU MANJI KUJIUZULU

Kufuatia Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa Klabu ya Yanga, kamati ya utendaji ya klabu hiyo inatarajiwa kukutana leo Jumatano kujadili suala hilo.
Akizungumza na SHUTIKALI, mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Omar Said alisema wamepokea barua hiyo kwa masikitiko kwa kuwa Manji alikuwa na mchango mkubwa klabu hapo lakini kwa kuwa Yanga ni taasisi kubwa basi wao watakutana na kutoa tamko.

“Tumepokea kwa masikitiko barua yake ya kuomba kujiuzulu, lakini kwa kuwa Yanga ina viongozi wake wengi na ina kamati ya utendaji, mimi niwaambie tu wanachama na mashabiki wa klabu hii kuwa hawatakiwi kuwa na papara wala hofu.

“Yanga ni taasisi kubwa na kwa kuwa yeye Manji alichaguliwa na wanachama, basi tukikutana ndiyo tutatoa tamko rasmi la kujibu barua yake,” alisema mjumbe huyo.

Alipoulizwa kujiuzulu kwa Manji kama kuna uhusiano wowote na mkataba ambao Yanga aimeingia na Kampuni ya SportPesa alisema:

“Hapana, katika barua yake amezungumza suala la afya, sidhani kama ni suala hilo.

“Unajua mimi nawapongeza wachezaji kutokana na kuonyesha moyo wa kupambana katika kipindi hiki kigumu ambacho mambo yalikuwa hayajatulia ndani ya klabu.”

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search