banner

May 14, 2017

MABILIONI YA SPORTPESA YAZUA KIZAAZAA SIMBA, HANS POPPE ATANGAZA KUJIONDOA KWENYE KAMATI YA USAJILI SIMBA

MABILIONI YA SPORTPESA YAZUA KIZAAZAA SIMBA, HANS POPPE ATANGAZA KUJIONDOA KWENYE KAMATI YA USAJILI SIMBA

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Zacharia Hans Poppe ametangaza kujiondoa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa kigogo huyo amefikia uamuzi huo kutokana na kuona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa, huku suala la mkataba wa Simba na Kampuni ya Sportpesa ukitajwa kuhusika.

Mtoa taarifa amenukuliwa akisema: “Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa.
"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka automatically katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili.
"Kilichomchukiza, kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema hana Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search