banner

May 15, 2017

NAHODHA WA SERENGETI BOYS APASUKA MFUPA

NAHODHA WA SERENGETI BOYS APASUKA MFUPA

Nahodha wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti boys, Issa Abdi Makamba, hatoweza kushiriki michuano ya AFCON U-17 inayofanyika huko Gabon kutokana na kuumia mguu kulikopelekea kupasuka kwa mfupa wakati akiwa katika moja ya mazoezi kujiandaa na michuano hiyo.
Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa ni kweli Abdi amepata majeraha hayo ambayo yatamsababisha kushindwa kushiriki michuano hiyo ambapo leo Mei 15 Serengeti Boys watamenyana na timu ya Mali.
“Ni kweli jambo la kusikitisha kidogo, kuwa nahodha wetu Abdi Makamba alipata mpasuko wa mguu juzi mazoezini akiwa peke yake kabisa. Na kwa mujibu wa taarifa za  madaktari yangu hatoweza kushiriki mashindano haya na jina lake tumeliondoa katika mashindano.”
“Tayari nafasi yake kwa vile tulikuwa na wachezaji wa akiba wameireplace nafasi hiyo. Imekuwa bahati mbaya kwa Issa Abdi mtu ambaye amepambana kwa miaka miwili kuiongoza hii timu kuhakikisha kuwa imefika mahali ilipofika Ataendelea na majukumu mengine kama Captain kuhamasisha..” alisema Shime.
Aidha madaktari wamesema kuwa Abdi atashindwa kucheza kwa muda wa miezi mitatu ili kuuguza majeraha aliyoyapata katika mguu wake.
Kocha huyo aliongeza kuwa kuumia kwa nahodha Abdi, hakutosanbabisha kushuka kwa kasi waliyonayo vijana wa Serengeti Boys na wanaamini kuwa watafanya vizuri na kupata ushindi katika michuano hiyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search