banner

May 20, 2017

PREMIER INAMALIZIKA KESHO, ARSENAL ISIPOSHINDA, SANCHEZ ANASEPA

PREMIER INAMALIZIKA KESHO, ARSENAL ISIPOSHINDA, SANCHEZ ANASEPA

Habari imejulikana kuwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexies Sanchez anaweza kuondoka kwenye timu hiyo baada ya mchezo wa kesho Jumapili.
Taarifa zimekuwa zikisema kuwa staa huyo anachotaka ni kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kama Arsenal watakosa nafasi hiyo kwenye mchezo wao wa mwisho wa Jumapili basi staa huyo atafungua mlango.

Sanchez bado hajasaini mkataba mpya na timu hiyo, huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza baada ya fainali ya Kombe la FA, Mei 27 dhidi ya Chelsea.

Inaaminika kuwa ushawishi wa fedha ndiyo unaweza kumfanya mchezaji huyo akabaki kwa kuwa anataka mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki ambazo bado Arsenal hawajawa tayari kuzitwaa.

Kwenye msimamo kwa sasa Arsenal wapo nafasi ya nne pointi moja nyuma ya Liverpool ambao kwenye mchezo wa mwisho watacheza na Middlesbrough ambao wameshashuka daraja na Arsenal watakuwa nyumbani kuvaana na Everton.

Hii ina maana ili Arsenal afuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya anatakiwa kushinda halafu Liverpool wapoteze au kutoka sare.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search