banner

May 24, 2017

SPORTPESA WAENDELEA KUFANYA YAO, SASA NI LIGI YA KENYA NA TANZANIA "SPORTPESA SUPER CUP"

SPORTPESA WAENDELEA KUFANYA YAO, SASA NI LIGI YA KENYA NA TANZANIA "SPORTPESA SUPER CUP"

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo imezindua ligi itakayojulikana kama SportPesa Super Cup.

Ligi hiyo itashirikisha timu nne kutoka Tanzania na Kenya ambayo itachezwa kutafuta bingwa na mshindi wa pili.


Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema ligi hiyo inatarajiwa kuanza  Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11.

“Utakuwa ni ushindani wa timu nne, kutoka Tanzania na Kenya. Hawa ni majirani na siku zote ni wapinzani wakubwa,” alisema.


Bingwa wa SportPesa Super Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 huku mshindi wa pili akipata dola 10,000.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search