banner

May 24, 2017

TAJIRI ANAYEIMILIKI ARSENAL AZUNGUMZIA KUHUSU KLABU HIYO KUUZWA

TAJIRI ANAYEIMILIKI ARSENAL AZUNGUMZIA KUHUSU KLABU HIYO KUUZWA

Mfanyabiashara mwenye hisa nyingi katika Klabu ya Arsenal, Stan Kroenke anasema kuwa hisa zake haziuzwi na hazijawekwa katika mauzo.
Kampuni hiyo ya Marekani ilitoa taarifa siku ya Jumatatu kufuatia ombi la pauni bilioni moja la kuinunua Arsenal.

Kampuni ya michezo na burudani ya Kroenke iliongezea kwamba itaendelea kuwa mwekezaji mkubwa wa Arsenal.

Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya Arsenal kushindwa kufuzu katika kinyang'anyiro cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Usmanov anamiliki asilimia 30 lakini siyo miongoni mwa bodi ya klabu hiyo inayofanya uamuzi.

Raia huyo wa Urusi aliyezaliwa Uzbekistan alisema mnamo mwezi Aprili kwamba Kroenke lazima achukue jukumu la msururu mbaya wa matokeo uwanjani.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search