banner

June 22, 2017

BEKI WA AZAM FC AMEMALIZANA NA YANGA ILA MKATABA WAKE NI KIKWAZO

BEKI WA AZAM FC AMEMALIZANA NA YANGA ILA MKATABA WAKE NI KIKWAZO

Taarifa kutoka vyanzo vya uhakika zinaeleza kuwa beki wa kushoto wa Azam FC, Gardiel Michael Mbaga amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili kujiunga na Klabu ya Yanga, lakini itabidi atasubiri hadi mzunguko wa pili kuanza kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Garidel anamaliza mkataba wake Azam FC, Desemba mwaka huu, maana yake atalazimika kusubiri hadi mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ndiyo aanze kucheza.
Gardiel ni miongoni mwa wachezaji waliopatikana kutokana na sera nzuri za uwekezaji kwenye soka ya vijana ndani ya Azam FC pamoja na akina Aishi Manula anayekwenda Simba, Mudathir Yahya anayekwenda Singida United na Farid Mussa anayecheza kwa mkopo DC Tenerife ya Hispania.
Na baada ya kusaini Yanga kufuatia kutemwa kwa Oscar Joshua, Gardiel atakwenda kupambana kujaribu kumpindua beki chaguo la kwanza wa timu hiyo, Mwinyi Hajji Mngwali.
Wakati huo huo: Kiungo Mudathir Yahya naye amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili, kufuatia kumaliza mkataba wake Azam FC.  Uongozi wa Azam umetoa baraka zake zote kwa Mudathir kuhamia Singida.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search