banner

June 05, 2017

GRIEZMANN ATOA KAULI YA KUHUSU KUTUA MANCHESTER UNITED

GRIEZMANN ATOA KAULI YA KUHUSU KUTUA MANCHESTER UNITED

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amethibitisha kuwa mipango yake ni kuendelea kuitumikia timu yake ya sasa baada ya adhabu yao ya kufungiwa kuendelea.
Straika huyo amekuwa akiwindwa na Manchester United lakini uamuzi wake huo unamaanisha kuwa dili limekuwa gumu na itabidi Man United watafute mpango mbadala.

Hivi karibuni Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ilitangaza kutupilia mbali rufaa ya Atletico iliyopinga kufungiwa kutosajili kutoka na kukiuka vipengele vya usajili kwa kumsajili mchezaji chini ya umri wa miaka 18 kinyume cha kanuni.

Akizungumzia majaaliwa yake alisema: “Nimeamua kubaki, halitakuwa jambo zuri kuondoka wakati huu.

“Tulikuwa na msimu mgumu, ni wakati wa kuwa na umoja kama timu.”

Atletico Madrid imefungiwa kutosajili hadi mwaka 2018 kutokana na kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) katika usajili.

Kauli hiyo inaweza kuwa changu kwa mashabiki wa Man United ambao walikwua na imani kuwa watampata mchezaji huyo kuongeza nguvu hasa kwa kuwa straika wao tegemeo Zlatan Ibrahimovic ni majeruhi anasumbuliwa na maumivu ya goti.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search