BARCA YATETA NA SEMEDO KWA HERUFI KUBWA

Nelson Semedo Benfica
Barcelona wapo katika mazungumzo yaliyochangamka na Nelsen Semedo wa Benfica, kwa mujibu wa  Record .
Semedo anaweza kupatakana kwa paundi milioni 69 kama bei iliyopangwa na klabu yake, lakini Barca wanakaribia kumnasa kwa paundi milioni 43.

MAN UTD YAANDAA DAU LA PERISIC

Perisic Fiorentina Inter Serie A
Manchester United wapo tayari kutoa dau la euro milioni 52 kwa ajili ya winga wa Inter Milan Ivan Perisic, Gazzetta dello Sport limeripoti.
United wanataka kuimarisha zaidi na kukifanya kipana kikosi chao na tayari wameshatenga dau la euro milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia.

LIVERPOOL YAWANYATIA SALAH & BALDE

HD Mohamed Salah
Liverpool bado wanaendelea na mazungumzo katika mchakato wao wa kuifukuzia saini ya Mohamed Salah kutoka Roma, pia wanavutiwa na Kieta Balde Diao kutoka Lazio, kwa mujibu wa ESPN .

CHELSEA WANAMTAKA ALVES

Dani Alves
Chelsea, Manchester City na Tottenham wanafikiria kumsajili Dani Alves majira ya joto, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mbrazili huyo anaaminika kuwa tayari kuondoka Juventus mwisho wa msimu huu, Conte akiwa shabiki wake mkubwa anataka kumleta Darajani ampe changamoto Victor Moses.

ARSENAL YAJIUNGA MBIO ZA MBAPPE

Kylian Mbappe Monaco
Arsenal nayo imeingia kwenye mbio za kuifukuzia saini ya nyota wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa  L'Equipe 
Kinda huyo amezivutia klabu nyingi Ulaya, Real Madrid na Manchester United zikiwa klabu zenye nafasi kubwa zaidi kuinasa saini yake.
Lakini Arsene Wenger akiwa amesaini mkataba mpya tena, Gunners wapo tayari kutoa hadi euro milioni 100 kumleta nyota huyo kinda uwanja wa Emirates. 

REAL MADRID YAANDAA £100M KUMSAJILI HAZARD

Eden Hazard Chelsea
Real Madrid wamejiandaa kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kumsajli Eden Hazard kutoka Chelsea, kwa mujibu wa  the Sun .
Miamba hao wa La Liga tayari wameshakutana na wawakilishi wa Hazard mara tatu katika harakati zao kumsajli mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kwa ada ya hatari ya kuvunja rekodi ya paundi milioni 100. Madrid wanaamini uwepo wa Zinedine Zidane unaweza kuwasaidia kumshawishi Hazard kuondoka Chelsea, lakini Antonio Conte hataki kumuuza mchezaji wake.

TOLISSO KWENYE RADA ZA CHELSEA

Corentin Tolisso Angel Di Maria PSG Lyon Ligue 1 19032017
Chelsea wanajipanga kumsajili kiungo wa Lyon Corentin Tolisso na wanaweza pia kumrejesha beki Kurt Zouma Ligue1 kama sehemu ya dili, L'Equipe  kimeripoti.
OL wapo tayari kufanya mazungumzo kuhusu Bertrand Traore, ambaye anaweza kutua Ufaransa kwa euro milioni 20.

NEWCASTLE WANAMTAKA ISMAILA SARR

Ismaila Sarr Metz PSG
Kinda wa Metz Ismaila Sarr amefurahia kupata nafasi kucheza ligi kuu ya Ufaransa msimu huu na anaweza kutua Newcastle, kwa mujibu wa L'Equipe .
Rafa Benitez anataka kumsajili winga huyo mwenye umri wa miaka 19 na timu yake imeshatoa ofa ya euro milioni 12, ingawa Metz wanataka euro milioni 15 kumwachilia.

MAN UNITED YAKATAA €60M ZA MADRID KUMUUZA DE GEA

David de Gea Manchester United
Manchester United wamekataa ofa ya euro milioni 60 kutoka Real Madrid kwa ajili ya kipa wao David de Gea, kwa mujibu wa Sky Sports News 
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akifuatiliwa sana na Real Madrid lakini United bado wamekuwa wazito kumuuza na wamesema hapana kwa mara nyingine dirisha la uhamisho linapokaribia kufunguliwa.

LEICESTER WANATAKA £50M KUMWACHIA MAHREZ

Riyad Mahrez Leicester City
Leicester City wamedhamiria kupata fedha nono kutoka kwa Riyad Mahrez na wametangaza ada yake kuwa paundi milioni 50, kwa mujibu wa Daily Star 
Mchezaji huyo hana utulivu baada ya kampeni za 2016-17 Ligi Kuu Uingereza, lakini Mbweha hawatamwachia kuondoka kwa bei rahisi.

JUVE WANATAKA KUMSAJLI SZCZESNY WA ARSENAL

Wojciech Szczesny Roma
Wojchiech Szczesny huenda akaendelea kubaki Serie A msimu ujao kwani Juventus wanaandaa kitita cha paundi milioni 14 kwa ajili ya kipa huyo wa Arsenal anayecheza Roma kwa mkopo, limeripoti Daily Mail 
Mlinda mlango huyo wa Poland ameonyesha uwezo mkubwa tangu alipotua Roma, akiwawezesha miamba hao wa Italia kufuzu Ligi ya Mabingwa baada ya kumaliza nafasi ya pili. 

LIVERPOOL YAMNYATIA SALAH

HD Mohamed Salah
Wakala wa Mohamed Salah amedokeza kuwa nyota huyo wa Roma yupo mbioni kutua Liverpool baada ya kubainisha kuwa alikuwa safarini kwenda Uingereza, kwa mujibu wa Express 

MBAPPE ANATAKA KWENDA MADRID

Kylian Mbappe Juventus Monaco Champions League
Nyota wa Monaco Kylian Mbappe anataka kujiunga na Real Madrid licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, kwa mujibu wa Marca .
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 ametajwa kuwa kwenye rada za Man City Pep Guardiola akitaka kumweka Mbappe kwenye kikosi chake cha kwanza moja kwa moja. Lakini Mfaransa huyo anataka kutua Real Madrid na atakataa fursa ya kutua Man City.

GRIEZMANN AITAARIFU ATLETI ANATAKA KUONDOKA

Antoine Griezmann
Antoine Griezmann ameuambia uongozi wa Atletico Madrid kuwa anataka kuondoka majira ya joto, kwa mujibu wa  Deportes COPE .
Manchester United wamekuwa kwenye harakati za kumsajili mchezaji huyo wa kimatifa wa Ufaransa, na huenda akatua kwenye kikosi hicho cha Jose Mourinho.

MOU AFANYA MAZUNGUMZO YA SIRI NA MORATA

Alvaro Morata, Dani Carvajal, Real Madrid
Jose Mourinho amefanya mazungumzo ya faragha na mshambulizi wa Real Madrid Alvaro Morata, kimeripoti  OkDiario .
Inadaiwa kuwa Milan ndiyo timu yenye uwezekano mkubwa wa kuipata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa dau la euro milioni 60, lakini bado Mourinho anaamini Muhispania huyo atakuwa namba 9 sahihi kwa Man United.

MILAN YATOA €60M KWA AJILI YA MORATA

Alvaro Morata Real Madrid La Liga
AC Milan watatoa euro milioni 60 kwa ajili ya mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kwa mujibu wa habari za  La Gazzetta dello Sport
Mshambuliaji huyo wa Kihispania tayari ameshakubali kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kwa mkataba wa euro milioni 8 kwa msimu.

LINDELOF KUIGHARIMU UTD £52M

Victor Lindelof Benfica
Manchester United wameambiwa watalazimika kutoa euro milioni 60 ambazo ni sawa na paundi milioni 52 kumsajili beki wa Benfica Victor Lindelof, kwa mujibu wa A Bola .

WENGER AONYWA KUHUSU USAJILI

Arsene Wenger Arsenal Chelsea FA Cup final 2017
Arsene Wenger ataonywa kuhusu tabia yake ya kusita kufanya usajili na bodi ya Arsenal katika kikao kitakachopitisha maamuzi ya kumpatia mkataba mpya leo, kwa mujibu wa Daily Mail .
Kumkosa Gonzalo Higuain 2013 ni miongoni mwa mifano ambayo Wenger alishindwa kufanya usajili ambao ulikuwa muhimu na wenye tija.

MAN UTD YAMFUATILIA BALE

Gareth Bale Real Madrid
Manchester United bado wanamtupia jicho Gareth Bale wakitaka kumsajili mchezaji huyo nyota wa Real madrid majira ya joto, Mundo Deportivo reports .
Ikiwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 hataanza kwenye mechi ya fainali Ligi ya Mabingwa, Meshetani Wekundu watazidi kuwa na imani ya kumsajili majira ya joto.

CHELSEA KUTUMIA £200M USAJILI MAJIRA YA JOTO

Antonio Conte Chelsea
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amepewa kitita cha paundi milioni 20 kufanya usajili majira ya joto, kwa mujibu wa  Daily Telegraph .
Bosi huyo anataka kuwasajili Virgil van Dijk, Romelu Lukaku na Tiemoue Bakayoko miongoni mwa shabaha yake.

RAFA ANAMTAKA REINA NEWCASTLE

Rafa Benitez anataka kufanya kazi na kipa wa Napoli Pepe Reina katika klabu ya Newcastle kwa mujibu wa  The Sun .

LYON YAMTOLEA OFA CHICHARITO

ATLETICO MADRID BAYER LEVERKUSEN JAVIER HERNANDEZ CHICHARITO CHAMPIONS LEAGUE 15032016
Lyon wametoa ofa ya euro milioni 12 kwa ajili ya mshambulizi wa Byer Leverkusen Javier Hernandez kwa mujibu wa  RMC .
Miamba hao wa Ligue 1 wanataka kuziba pengo la Alexandre Lacazette.

MAN CITY YAMTOLEA €130M MBAPPE

Kylian Mbappe Juventus Monaco Champions League
Manchester City wametoa ofa ya rekodi ya dunia ya paundi milioni 114 kwa ajili ya kinda wa Monaco Kylian Mbappe, limeripoti  Telefoot .

MAN UTD HAITAMNUNUA PERISIC

Ivan Perisic
Manchester United wamepungukiwa euro milioni 15 katika dau lao la kutaka kumsajli Ivan Perisic wa Inter Milan kwa mujibu wa Calcio Mercato

STOKE YAMTENGEA DAU ROONEY

Wayne Rooney Manchester United
Stoke City wametoa ofa wakitaka kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Manchester United Wayne Rooney kwa mujibu wa Daily Mirror.
Rooney alishakataa kwenda China Januari na anatarajiwa kuondoka Old Trafford msimu huu.

UTD NA CHELSEA VITANI KUMSAJILI LUKAKU

Romelu Lukaku Everton Premier League
Romelu Lukaku wa Everton ameamsha vita kali baina ya Chelsea na Manchester United zinazotaka kumsajili majira ya joto.

ARSENAL YAONGOZA MBIO ZA KUMWANIA BELOTTI

Andrea Belotti Torino Crotone Serie A
Arsenal wanataka kumsajili Andrea Belotti kutoka Torrinho lakini watakumbana na ushinda kutoka kwa Chelsea na Manchester United, imeripotiwa na The Sun.

AC MILAN YAJIUNGA MBIO ZA KUMFUKIZIA DEMBELE

HD Moussa Dembele Celtic
AC Milan imeungana na Arsenal, Chelsea na Tottenham kuiwania saini ya mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele, limeripoti Express.

GUARDIOLA KUSAJILI WATOTO WA BARCA

Pep Guardiola Manchester City
Pep Guardiola anataka kuwasajili vijana hatari kutoka Barcelona, Pablo Moreno, Nico Gonzalez na Ansu Fati katika timu ya Man City.

MOURINHO AISHURUTISHA MAN UTD KUMSAJILI KEANE

Michael Keane Burnley
Jose Mourinho ameitaka bodi ya Manchester United kufanya haraka iwezekanavyo kumsajili Michael Keane kutoka West Ham united.

MORATA ANATAKA KUTIMKIA MILAN

Alvaro Morata Real Madrid La Liga
Alvaro Morata yu mbioni kurejea Ligi ya Italia, awamu hii atatua AC Milan kwa mujibu wa Sky Sport Italia. ( via  Football Italia 

NEYMAR NJE VERRATTI NDANI BARCELONA

Neymar, Verratti split
Barcelona wapo tayari kuachana na Neymar ili waweze kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Marco Verratti kwa mujibu wa  Yahoo .

UNITED INAWATAKA GRIEZMANN, LUKAKU & BELOTTI

Romelu Lukaku Everton Premier League
Jose Mourinho yupo tayari kutumia fedha za kutosha kuiboresha safu yake ya mashambulizi Manchester United, kwa mujibu wa Daily Mail .
Mashetani Wekundu wanataka kumsajili Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, Andrea Belotti wa Torino na Romelu Lukaku wa Everton kuziba pengo la Zlata Ibrahimovic na Wayne Rooney. Beki wa Burnley Michael Keane pia yumo kwenye rada.

MOURINHO ANAMTAMANI LUCAS

Lucas Moura PSG Bastia Ligue 1 06052017
Jose Mourinho anatarajia kusajili winga wa kulia majira ya joto na amemgeukia Lucas Moura wa Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa SportWitness .
Bosi huyo wa Manchester United atajaribu kwa mara nyingine kumsajili Mbrazili huyo baada ya kupata ugumu kuishawishi Chelsea kumuuza Willian.

INTER WANAWATAKA JAMES & PEPE

James Rodriguez Real Madrid Granada LaLiga 06052017
Inter wanataka kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa Real Madrid Pepe na James Rodriguez uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa Sportitalia .
Kadhalika Manchester United nao wametajwa kuifukuzia saini ya Mcolombia James ambaye anataka kuondoka Madrid majira ya joto baada ya kushindwa kumshawishi Zinedine Zidane.