banner

June 15, 2017

KASEJA AZUNGUMZIA UAMUZI WA JOHN BOCCO KUONDOKA AZAM

KASEJA AZUNGUMZIA UAMUZI WA JOHN BOCCO KUONDOKA AZAM

Kipa mkongwe Juma Kaseja ametoa maoni yake kuhusu wachezaji wa soka wa Tanzania kwa kusema wachezaji waandamizi hawapewi heshima wanayostahili kwenye klabu zao licha ya kujitolea na kuvitumikia kwa moyo.
Kauli hiyo ameitoa baada ya Azam FC kumtosa aliyekuwa nahodha wao John Bocco kufuatia mkataba wa mchezaji huyo kumalizika huku kuondoka kwake kukizua utata ikionekana kama hakuondoka vizuri.
“Sijui kuna nini kimetokea ndani ya Azam kwa sababu hata mimi nasikia tu kama mnavyosikia ninyi kwamba, kuna utaratibu umewekwa hakuna kusajili mchezaji kwa zaidi ya shilingi milioni 15 lakini tunasikia Mbaraka kachukua zaidi ya shilingi milioni 15.

“Sasa mimi nadhani kuna vitu vimetokea kwenye mpira wa Tanzania kwa kutaka kuwaondoa wachezaji waandamizi kwenye timu na hivi vitu havipo Azam tu, vipo kwenye mpira wa Tanzania, Azam wamevitoa kwenye hizi timu mbili na kuvipeleka kwao.

“Watu hawataki kuwapa heshima, lazima wawape heshima wachezaji, Bocco ni mchezaji mkubwa ndani ya Azam wanatakiwa wampe heshima yake. Hata kama kulikuwa na matatizo ya mambo ya fedha na uchumi wangekaa chini wazungumze nae.

“Bocco na yeye ni binadamu kama miaka yote kachukua fedha nyingi anawezaje kukataa kwa mwaka mmoja kama ameeleweshwa kuwa timu haiku vizuri kuhusu hali ya timu kiuchumi?

“Lakini kwa mchezaji kama Bocco ambae ameshajitolea sana kwenye timu hata yeye hawezi kuwa na furaka kwa sababu anaona kama amedharaulika na hivyo ni vitu ambavyo wamefanyiwa watu wengi sema kwa Azam ndio mchezaji wa kwanza lakini kwenye hizi timu nyingine watu wamefanyiwa sana.”

Bocco amesha saini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Simba kuanzia msimu ujao wa 2017/2018.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search