banner

June 10, 2017

USAJILI ULIOBUMA KATIKA LIGI KUU BARA, SIMBA, YANGA NDANI PIA

USAJILI ULIOBUMA KATIKA LIGI KUU BARA, SIMBA, YANGA NDANI PIA

Katika mashindano yoyote kuna wa kwanza ambaye ni mshindi na wa mwisho, pamoja na wachezaji waliofanya vizuri Ligi kuu wapo walifanya vibaya.
Hawa ni wachezaji ambao usajili wao unaweza kusema haukuwa na faida kubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika hivi karibuni wa 2016/17:
10. Fedric Blagnon
Kiwango chake kimekuwa ni cha kawaida tofauti na matarajio ya wengi, licha ya U-pro wake ila ameshindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Simba, Muivory coast huyu licha ya kutumika pesa nyingi kwenye usajili wake hajafikisha hata mabao manne kwenye Ligi. Japokuwa alionekana katika matukio muhimu hasa katika mechi mbili zilizoihusisha timu yake dhidi ya Mbao FC. 

9. Mrisho Ngassa
Mmoja wa winga bora kuwahi kutokea hapa nchini, alisajiliwa na Mbeya City akitokea Afrika kusini dirisha dogo, tangu atue Mbeya Ngassa ameshindwa kuonesha ubora wake, amemaliza Ligi bila kufunga goli lolote.

8. Yahaya Mohammed
Mshambuliaji kutoka Azam, alisajiliwa kwa fedha nyingi msimu uliopita kwa matarajio ya kuja kuongeza nguvu kwenye idara ya ushambuliaji, Mohammed ameshindwa kuonesha makali take tangu atue nchini mwisho ameishia benchi tu.

7. Samuel Afful
Mghana wa Azam, Afful ni moja ya usajili uliyo itia klabu hasara kwani ameshindwa kuonyesha thamani yake, amemaliza msimu bila goli na kuporwa namba na wazawa.

6. Pastory Anthony
Alijiunga na Simba akitokea Stand United, Pastory alitazamiwa kuleta changamoto kwa kina Ajibu na Mavugo, tofauti na matarajio ya wengi mshambuliaji Hugo ameshindwa kuonesha makali kama ya huko nyuma.

5. Hamad Juma
Ametokea Coast Union na kuja Simba kwa ajili ya kurithi mikoba ya Kessy aliye jiunga na Yanga, matokeo yake mlinzi huyo amekuwa akiishia jukwaani akiwatazama wenzake.

4. Danny Mrwanda
Mkongwe ameshindwa kuwa na msaada ndani ya Kagera na kushuhudia namba yake ikiporwa na machipukizi kina Mbaraka Yusuph na Edo Christopher, usajili wa Mrwanda haukuwa na faida ndani ya Kagera ndani ya uwanja.

3. Justine Zulu
Kipindi anajiunga na Yanga ajitokea Zambia alibatizwa majina lukuki kama "mkata umeme", ila kiungo huyo mkabaji hakuna jipya aliloongeza ndani ya Yanga, Zulu anatazamiwa kutemwa kwa msimu ujao.

2. Atupele Green
Mfungaji bora wa kombe la shirikisho Fa msimu 2015/2016, Atupele alijiunga na JKT Ruvu msimu uliomalizika, tangu atue JKT Ruvu, Atupele ameshindwa onesha makali yake na kushindwa kuinusuru klabu yake kwenye janga la kushuka daraja.

1. Hussein Shariff
Maarufu kama "Cassilas", nyanda huyo alitokea Mtibwa na kujiunga na Kagera msimu uliopita, Shariff ameishia kucheza mechi chache za mzunguko wa kwanza tu kabla ajatemwa na klabu kwa tuhuma za kujihusisha na upangaji wa matokeo.


CHANZO: GOAL.COM

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search