banner

July 05, 2017

MASTAA WALIOONDOKA SIMBA, WAKATUA YANGA WAKANG’ARA

MASTAA WALIOONDOKA SIMBA, WAKATUA YANGA WAKANG’ARA

Usajili wa klabu za Simba na Yanga unaohusisha mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine kati ya hizo mara nyingi huwa unaambatana na gumzo kubwa.
Hivi karibuni imeshuhudiwa Ibrahim Ajibu ikidaiwa kuwa anaweza kuwa miongoni mwa nyota wapya watakao jiunga na Klabu ya Yanga kwa ajili ya msimu mpya  wa 2017/2018 akitokea Simba.

Baada ya kuwa na misimu miwili mizuri ndani ya Simba, sasa wapenzi na mashabiki wanataka kuona kama Ibrahim Ajibu atafata nyayo za  baadhi ya mastaa ambao wameng'ara Yanga baada kutoka Simba. 

Hawa ni baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza Simba na kuamua kujiunga Yanga na kwenda kupata mafanikio katika soka la Tanzania wakiwa na jezi ya Yanga.

Amiss Tambwe
Mrundi huyu alisaini Simba mwaka 2013 baada ya kuibuka mfungaji bora kombe la kagame, alitupiwa vilago ndani ya Simba baada ya kudumu kwa msimu mmoja licha ya kuibuka  kinara wa magoli Ligi Kuu, alitua Yanga mwaka 2014 na kufanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi baada ya kufanikiwa kufunga magoli zaidi ya sabini katika mashindano yote, kadhalika kuisaidia klabu kushinda mataji mbali mbali 

Kevin Yondani
Alisaini Yanga 2012 baada ya kucheza Simba takribani misimu 3, Yondani ndani ya  Yanga amefanikiwa kutengeneza safu bora ya ulinzi  kwa kipindi chote na kuifanya klabu  kushinda medali zaidi ya 6 katika mashindano mbali mbali ,  Ligi Kuu bara,klabu bingwa Afrika Mashariki na kati,  kombe la ngao ya hisaini na kuiwezesha Yanga kucheza hatua ya makundi mwaka kwa mwaka jana chini ya mwalimu Hans Van Pluijm.

Athumani Mambosasa
Kipa bora kuwahi kutokea kwenye nchi hii,baada ya kutamba kwa mda mrefu na Simba kama akina Deo Njohole,Hamiss Gaga.Athumani Mambosasa aliamua kujiunga na Yanga .Watu wengi wakiamini hatashindwa Yanga lakini ilikuwa tofauti ,alifanikiwa kucheza kwa kiwango kikubwa pale Yanga.

Athumani Idd Chuji
Mmoja wa viungo bora wa ulinzi waliowahi pita ndani ya klabu ya Yanga, tangu aondeke Jangwani miaka zaidi ya 6 klabu imekuwa ikihaha kutafuta mrithi sahihi ambaye ataweza kutimiza majukumu ya ulinzi kwa asilimia kubwa, alijiunga na Simba baada ya kuonekana kwenye Ligi daraja la kwanza akiwa na klabu ya  Polisi Dodoma , Chuji hakudumu sana na Simba na kuamua kujiunga na Yanga , kiungo huyo ndani ya Yanga alifanikiwa kudumu takribani misimu 8 na  kushinda  karibu kila kitu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati akiwa ndani ya uzi wa Yanga.

Ally Mustapha 'Barthez'
Amedumu Yanga zaidi ya mika 7 sasa tangu atoke Simba na kuamua kujiunga na Wanajangwani, mlinda mlango huyo ameiwezesha klabu kushinda mataji mbali mbali ya ndani na nje ya nchi kwa kipindi chote alichodumu Yanga.

CHANZO: GOAL

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search