banner

July 01, 2017

SIMBA HAIJATOSHEKA TU, KOCHA JOSEPH OMOG ASEMA BADO ANAWATAKA HAWA…

SIMBA HAIJATOSHEKA TU, KOCHA JOSEPH OMOG ASEMA BADO ANAWATAKA HAWA…

Kikosi cha Simba kimekamilisha mchakato wa kuwasajili wachezaji kadhaa ambao wametua kutokana na mapendekezo ya Kocha Joseph Omog ambaye yupo nchini kwao Cameroon kwa ajili ya mapumziko lakini bado kuna wengine wanahitajika.
Mpasa sasa Simba kupitia kamati yake ya usajili chini ya Mwenyekiti Zakaria Hans Poppe, imewasajili wachezaji kadhaa ambao walikuwa wameorodheshwa na Mcameroon huyo akiwahitaji kwenye kikosi chake.

Wachezaji hao ni Emmanuel Okwi, John Bocco, Shomari Kapombe, Ally Shomary, Yusuph Mlipili, Jamal Mwambeleko pamoja na Emmanuel Mseja lakini Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanahitaji wachezaji wengine katika nafasi za ushambuliaji na mlinzi wa kati, na baada ya hapo watakuwa wamemaliza usajili wao ambapo wataanza masuala ya kambi.

“Licha ya usajili huu tulioufanya bado kocha ametuagiza kuleta silaha nyingine mbili kwenye maeneo ya ushambuliaji na beki wa kati baada ya hapo zoezi zima tulitalifunga na kuangalia mambo mengine.

“Tunaendelea kufanya uchunguzi ni nani tumsajili kwenye nafasi hizo na tukikamilisha basi watajiunga na sisi kama ambavyo tumefanya kwa wachezaji wengine ambao wamepita,” alisema Kaburu kabla ya kupata matatizo yaliyomfikisha mahakamani jana.

CHANZO: CHAMPIONI

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search