banner

July 22, 2017

SIMBA WAIPIGIA MAGOTI AZAM FC KWA MANULA

SIMBA WAIPIGIA MAGOTI AZAM FC KWA MANULA

ipa wa Azam FC, Aishi Manula.
 UONGOZI wa Klabu ya Simba, umeipigia magoti Azam FC imruhusu Aishi Manula aweze kushiriki mazoezi na klabu hiyo mapema kwa kuwa bado ana mkataba wa mwezi mmoja na timu hiyo.
Inadaiwa kuwa Manula ameshamalizana na Simba kwa mkataba wa miaka miwili lakini hataweza kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa kuwa bado mkataba wake na Azam FC haujamalizika.
Taarifa ambazo gazeti hili limezipata ni kuwa uongozi wa Simba umeiomba Azam FC kumruhusu Manula mapema ili akafanye mazoezi na kikosi hicho kilichopo Afrika Kusini ili kuepuka kesi kama ilivyokuwa kwa Hassan Kessy alivyokwenda Yanga.
Ulipotafutwa uongozi wa Azam FC kuzungumzia suala hilo ulisema kwa upande wao wanatambua kuwa Manula ni mchezaji wao hadi pale atakapomaliza mkataba na si vinginevyo.
“Manula bado ni mchezaji wetu hadi atakapomaliza mkataba wake, pia yeye mwenyewe ndiye anatakiwa aseme kama amemaliza mkataba ama la, lakini taarifa za Simba kufanya mazungumzo bado hazijanifikia,” alisema Mwenyekiti wa Azam FC, Idrisa Nassor.
Stori: Khadija Mngwai | Championi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search