banner

July 22, 2017

YANGA YASHUSHA MASHINE NYINGINE JANGWANI

YANGA YASHUSHA MASHINE NYINGINE JANGWANI

Katika kile ambacho kinaonekana kweli mambo yanaendelea kuwa mazuri upande wa Jangwani, habari nzuri ni kuwa,
Yanga imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji chipukizi, Baruan Yahya kwa mkataba wa miaka miwili.
Ofisa Habari Msaidizi wa Yanga, Godlisten Anderson Chicharito alisema wamemsajili chipukizi huyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Chicharito amesema mchezaji huyo awali alikuwa akisoma nchini Uganda lakini ameshahitimu kidato cha sita mwaka jana, ambapo amekubali kusaini Yanga na kuipa kisogo ofa ya kupewa uraia wa Uganda ili acheze kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.
Aidha, inaelezwa kuwa mchezaji huyo alikuwa akiichezea Lipuli katika maandalizi ya msimu ujao akiwa anafanya majaribio na tayari alishacheza mechi kadhaa za kirafiki.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search