banner

August 23, 2017

LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: YANGA 0 VS 0 SIMBA (SIMBA WAMESHINDA NGAO YA JAMII KWA PENALTI 5-4)

LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: YANGA 0 VS 0 SIMBA (SIMBA WAMESHINDA NGAO YA JAMII KWA PENALTI 5-4)


YANGA
1.Yondani (KOSA)
2.Tshishimbi (PATA)
3. Kamusoko (PATA)
4. Ajibu (PATA)
5. Ngoma (PATA)

1. Mahadhi (KOSA)




SIMBA
1. Mwanjale (PATA)
2. Okwi (PATA)
3. Niyonzima (PATA)
4. Kichuya (PATA)
5. Zimbwe (KOSA)



1. Mo Ibrahim (PATA)

DAKIKA 90 ZIMEKAMILIKA, SASA NI MKWAJU YA PENALTI
Dk 90+2 Niyonzima anamchambua Gadiel, anaachia mkwaju mkali kabisa lakini juuuuuuuu
Dk 90+2 Gadiel anafanya kazi ya ziada, anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Yanga wanaokoa
Dk 90+1, Simba wanapata kona hapa, inachongwa na Kichuya lakini mpira unakwenda nje, goal kick 


DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90 Simba wanaendelea kumiliki mpira lakini hawana malengo yanayotimia langni mwa Yanga ambao wako makini kiulinzi
SUB Dk 88, Mohamed Zimbwe Jr, anaingia kuchukua nafasi ya Nyoni ambaye ameumia
Dk 88 sasa, Nyoni yuko chini pale anatibiwa, mchezo umesimama 


SUB Dk 87, Yanga wanamuiginza Hassan Kessy anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul
KADI Dk 87 Yondani analambwa kadi ya njano hapa
Dk 85 sasa, Simba ndiyo wamemiliki mpira kwa muda mrefu zaidi lakini wajanja kuipita ngome ya Yanga
Dk 81, Mo Ibrahim, lakini kipa wa Yanga anafanya kazi kubwa kuokoa mpira huo, anamgonga Vicent, yuko chini
anatibiwa
Dk 80, Simba wanapata kona, inachongwa, Kichuya anajaribu lakini Yanga wanaokoa
Dk 79 Martin anaingia na kuachia mkwaju mkali, Manula anaokoa lakini mwamuzi anasema ilikuwa faulo
SUB Dk 78 Mohamed Ibrahim anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru
Dk 77 Tshishimbi ameachia shuti kali hapa lakini hakulenga lango


Dk 76, umbali wa takribani mita 25 lakini hakulenga lango
Dk 75, Gadiel anatoka katika nafasi yake, anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira miguuni kwa Liuzio ambaye kama angepiga, yangekuwa mengine
SUB Dk 73 Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Raphael Daud
SUB Dk 72 Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo upande wa Simba
Dk 72, Martin anaachia krosi safi kabisa langoni mwa Simba, lakini hakuna mtu
Dk 69 sasa, mpira umebaki katikati mrefu na inaonekana kutakuwa na shambulizi la kushitukiza upande mmoja litakalozua madhara

Dk 65, Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza, mabeki wa Simba wamezidiwa ujanja, lakini Manula anatoka na kuokoa Dk 62, Ajibu anamfanyia madhambi Shomari, mwamuzi anampa onyo kwa mdomo tu akimsisitiza kutulia Dk 60, mechi bado inaonekana haina spidi kali kama ambavyo ilitarajiwa. Lakini Yanga wanaonekana kuna kitu wanatafuta na hasa kwa shambulizi la kushitukiza kwa kuwa wanajaza wachezaji wengi nyuma kwa ulinzi na Simba wanaonekana kujisahau mara kadhaa Dk 56, Okwi anamzidi kasi Yondani, anabaki yeye na kipa lakini Kipa Mcameroon anafanya kazi nzuri kabisa, anaokoa miguuni mwa Okwi

Dk 53, Kamusoko anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini unapita juu ya lango  Simba, angelenga ingekuwa hatariiii
KADI DK 50, Kadi ya tatu ya mchezo, Niyonzima analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Juma Abdul aliyempokonya mpira
Dk 48, krosi fupi ya Nyoni, Mavugo anaruka peke yake na kupiga kichwa safi lakini Goal Kick
Dk 47, Okwi anaachia mkwaju mkali hapa lakini gadiel anaokoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa
DK 46, Juma anamimina krosi safi kabisa lakini kipa Manula anadaka vizuri kabisa
Dk 45, Mechi imeanza na Simba wanafanya shambulizi kali, Okwi anaingia lakini Youthe anaokoa vizuri kabisa hapa

MAPUMZIKO


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44 sasa, mpira unachezwa katikati ya uwanja, hakuna mashambulizi makali
Dk 41, Simba wanajibu shambulizi na kupata konaaaa, inachongwa na Kichuya na Niyonzima anaachia mkwaju mkali sana, goal kick
Dk 41, Yanga wanafanya shambulizi lakini Manula anatoka na kuuwahi mpira
Dk 40, krosi nzuri ya Nyoni, Mavugo anashindwa kulenga hapa
KADI Dk 38, kadi ya pili ya mchezo wa leo, inakwenda kwa Juma Abdul baada ya kumuangusha Kotei
Dk 35, pasi nzuri ya Niyonzima, Mavugo anapiga krosi, Yondani anapiga kichwa na kuwa kona, Yanga wanaokoa vizuri kabisa
Dk 33, Mavugo anageuka vizuri na kuachia mkwaju mkali hapa lakini Yondani anafanya kazi ya ziada
Dk 32, Simba wanapata kona ya kwanza baada ya kufanya shambulizi, inachongwa hapa na Niyonzima lakini Yanga wanaokoa vizuri hapa

Dk 31 kadi ya kwanza ya njano inatoka, MWanjale anafanya upuuzi kwa kupiga mpira chini kwa nguvu wakati filimbi ilishapulizwa
Dk 29 sasa, kidogo presha ya mchezo imehamia tena katikati kila timu ikionekana kutulia na kutaka kujipanga
Dk 27, Yondani anamdhibiti Mavugo hapa, analazimika kufanya faulo, inapigwa kwenda Simba

Dk 24, Martin anaachia mkwaju mkali hapa akipokea pasi ya Kamusoko, lakini hakulenga lango
Dk 23 Kipa Rostand, anafanya kazi nzuri kwa kudaka mpira wa juu wa krosi wa Nyoni
Dk 22, Ngoma anaingia vizuri kabisa lakini Mwanjale anafanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 22 sasa, Yanga wanaonekana kujilinda zaidi huku Simba wakiwa wameshambulia zaidi lakini ukiangalia difensi ya Simba inaonekana kuachia nafasi ambazo Yanga wakiwa makini wanaweza kuzitumia hasa kwa pasi za kupitisha

Dk 20, Okwi anaingia tena, anaachia mkwaju hapa lakini Yondani anaiokoa vizuri kabisa Dk 18, Niyonzima aanaingia na kuchambua vizuri, lakini basi aliyompa Muzamiru anapaisha buuuuu

Dk 16, Simba wanatangeneza nafasi nzuri zaidi, krosi ya Nyoni, Dante anaonekana kuzubaa na Mavugo anapiga kichwa lakini hakulenga
Dk 15 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna shambulizi kali


Dk 10, Niyonzima anachambua msitu, lakini Ngoma anasema hapana anamuweka chini hapa, faulo
Dk 9, Manula anamuwahi Ngoma na kuutoa mpira nje unakuwa wa kurusha
Dk 8, Tshishimbi anapiga kanzu katikati ya uwanja na kutoa pasi fyongo, Okwi anauwahi lakini Yanga wanakuwa makini, wanaokoa 

Dk 7, Gadiel anaingia vizuri na kuachia krosi safi, Shomari anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Juma, Manula anafanya kazi ya ziada na kuokoa

Dk 4, Muzamiru anaachia shuti kali hapa lakini Youthe anadaka kwa ufundi kabisa na kuanza vizuri hapa
Dk 3, kona ya kwanza ya mchezo, anakwenda kuichonga Gadiel hapaa, Simba wanaokoa na unakuwa mpira wa kurusha
Dk 2, Mbonde analazimika kumuweka Mbonde chini na Yanga wanapiga mpira wa adhabu kupitia Gadiel, kona
Dk 2 inaonekana bado kuna hali ya kuhofiana kidogo lakini Yanga wanataka kuchanganya kwa kuanza kwa kasi
Dk 1, mechi imeanza na Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kukanyaga na kuanza mpira


Shangwe ni nyingi kutoka pande zote, idadi ya mashabiki ni kubwa.
Mchezo umeanza.
Timu zinaingia uwanajani, muda wowote mchezo utaanza.
Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita, wapo uwanjani kukipiga dhidi ya Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la FA katika mchezo wa Ngao ya Jami kuukaribisha msimu wa 2017/18.
Kikosi cha Simba kinachoanza leo
1. Aishi Manula
2. Ally Shomari
3. Erasto Nyoni
4. Salim Mbonde
5. Method Mwanjale
6. James Kotei
7. Shiza Kichuya
8. Mzamiru Yassin
9. Laudit Mavugo
10. Emanuel Okwi
11. Haruna Niyonzima
WALIOPO BENCHI
1. E. Mseja
2. M. Tshabalala
3. Juuko M
4. J. Mkude
5. M.Kazimoto
6. J Luizio
7.MO Ibrahim

Kikosi cha Yanga
1.Rostand Youthe
2. Juma Abdul 
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vicent 
5. Kelvin Yondani
6. Papy Tshishimbi
7. Raphael Daud
7. Thaban Kamusoko
9. Ibrahim Ajibu
10. Donald Ngoma 
11. Emmanuel Martin
WALIOPO BENCHI

Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Haji Abdallah, Mwinyi Haji, Juma Makapu, Yusuph Mhilu, Juma Mahadhi 

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search