banner

August 24, 2017

NIYONZIMA AFICHUA SIRI YA KUAMUA KUICHEZEA SIMBA, WALA SIYO USHAWISHI WA FEDHA

NIYONZIMA AFICHUA SIRI YA KUAMUA KUICHEZEA SIMBA, WALA SIYO USHAWISHI WA FEDHA

Kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima amesema kuwa mbali na soka yeye pia ana kipaji cha juu katika uimbaji lakini akaenda mbele zaidi kwa kutaja kitu kilichosababisha aendelee kubaki nchini kucheza soka.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Niyonzima kwanza alisema anafurahia kuwepo Simba na Tanzania kwa jumla kwa kuwa siri kubwa ni nchi kuwa na amani ambapo hata yeye anajihisi kuwa na amani na mwenye furaha, chochote anachofanya anahisi yupo nyumbani.
Amedai kuwa fedha siyo chachu ya yeye kuwepo Tanzania bali amani, kwani ukiwa na fedha hauna amani ni sawa na bure.
“Mimi ni muimbaji, naweza kuingia studio na kuimba kabisa, lakini watu wengi hawajui hilo,” alisema Niyonzima.
Kuhusu uwepo wake Tanzania, Niyonzima ambaye ni raia wa Rwanda alisema: “Chochote ninachofanya nahisi nipo nyumbani, nikiwa Tanzania nimepata watoto, sijawahi kukaa nchi nyingine muda mrefu tangu nilivyoanza soka kama ilivyo hapa, hivyo nina amani kubwa kuwepo Tanzania.”

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search