banner

August 20, 2017

TETESI KUBWA ZA USAJILI WA SOKA BARANI ULAYA

TETESI KUBWA ZA USAJILI WA SOKA BARANI ULAYA

Kocha wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutumia pauni milioni 200 kuwasajili Danny Drinkwater, 27, kutoka Leicester,
kiungo wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, 24, na mabeki watatu wa Southampton, Virgil Van Dijk, 26, Cedric Soares, 25, na Ryan Bertrand, 28. (Express)
Chelsea wamemuulizia beki wa kati wa Tottenham Toby Alderweireld, 28, ambaye mazungumzo yake na Spurs kuhusu mkataba mpya yanasuasua. (Sunday Times)
Baada ya kumkosa Danny Drinkwater, meneja wa Chelsea sasa atamgeukia Grzegorz Krychowiak wa PSG. (Sun)
Atletico Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili Diego Costa kutoka Chelsea. (Daily Mail)
Diego Costa amekataa kwenda kwa mkopo katika timu za SIPG na Tianjin Quanjian za China ambapo angelipwa pauni milioni 13 kati ya sasa hadi mwezi Novemba. (Sun)
Barcelona watalipa pauni milioni 36.5 za kutengua kipengele cha uhamisho cha Jean Michel Seri, 26, na huenda wakakamilisha usajili wake ifikapo Jumatatu kutoka Nice. (Mundo Deportivo)
Barcelona wamewaambia Liverpool wana hadi siku ya Jumapili kukubali au kukataa dau la pauni milioni 118 la kutaka kumsajili Philippe Coutinho, 25, vinginevyo dau hilo litaondolewa mezani. (Times)
Barcelona wameweka usajili wa Philippe Coutinho kuwa kipaumbele na wanafanya kila jitihada kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Sport)
Barcelona watapanda dau jipya la pauni milioni 130, ingawa Liverpool wanasema thamani ya Philippe Coutinho ni pauni milioni 140. (Express)
Luis Suarez amewaambia Barcelona kuwa kumsajili Philippe Coutinho "sio dawa" ya matatizo waliyonayo sasa hivi. (Liverpool Echo)
Paris Saint-Germain hatimaye wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 182. (Mundo)
Newcastle wanafikiria kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 28. (Mirror)
Manchester United, Arsenal na Liverpool zinamtaka Julian Draxler, 23, wa PSG. (Mirror)
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amesema mshambuliaji Ousmane Dembele atauzwa kwa bei inayofaa. (FourFourTwo)
Barcelona watalazimika kutoa pauni milioni 137 pamoja na marupurupu juu ikiwa wanataka kumsajili Ousmane Dembele, 20. (RAC 1)
Arsenal wamewapa AC Milan nafasi ya kumsajili kiungo Jack Wilshere. (Corriere dello Sport)

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search