banner

August 23, 2017

YANGA Vs SIMBA NI LEO, LAZIMA UPANDE MMOJA UTOKE UNALIA TAIFA

YANGA Vs SIMBA NI LEO, LAZIMA UPANDE MMOJA UTOKE UNALIA TAIFA

Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana leo Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo shughuli inatarajiwa kuwa pevu baina ya pande hizo mbili.
Mchezo huo ambao utatangazwa mubashara na kituo cha redio cha SIBUKA FM ni wa kuukaribisha msimu wa 2017/18 ambapo Kocha Mzambia wa Yanga, George Lwandamina akiwa na rekodi ya kufungwa mechi zote mbili zilizopita alipokutana na watani hao wa jadi.
Tangu Lwandamina achukue nafasi ya Hans van der Pluijm, Desemba mwaka jana hajawahi kupata ushindi dhidi ya Simba licha ya kuwa aliiongoza Yanga  kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita.
Januari 10, mwaka huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilifungwa kwa penalti 4-2 na Simba baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Februari 26, mwaka huu, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-1 wafungaji wao wakiwa ni Laudit Mavugo dakika ya 66 na Shiza Kichuya dakika ya 81 huku lile la Yanga likiwekwa wavuni na Simon Msuva katika dakika ya 5.
Kila timu ina wachezaji kadhaa wapya, upande wa Simba kuna Aishi Manula, Said Mohammed, Erasto Nyoni, Ally Shomary, Salim Mbonde, Jamal Mwambeleko, Yussuf Mlipili, Paul Bundala, Shomary Kapombe, John Bocco, Nicholas Gyan na Emmanuel Okwi.
Wachezaji wapya ndani ya Yanga ni Youthe Rostand, Ramadhan Kabwili, Gardiel Michael, Abdallah Haji ‘Ninja’, Papy Kabamba Tshishimbi, Raphael Daudi, Pius Buswita na Baruan Akilimali.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search