banner

August 21, 2017

YANGA Vs SIMBA SASA KUPIGWA SAA 11 JIONI, SIYO SAA 10 JIONI

YANGA Vs SIMBA SASA KUPIGWA SAA 11 JIONI, SIYO SAA 10 JIONI

Siku moja kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema mechi  hiyo ambayo itawakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba inatarajiwa kuanza saa 11 jioni badala ya saa 10: Jioni.
Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amezungumzia juu ya mabadiliko hayo ya ratiba ya mchezo huo kusogezwa kwa saa moja zaidi ambapo pia alitangaza na viingilio kuwa ni Sh 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, Sh 10,000 kwa viti vya rangi ya Orange na Sh 20,000 kwa VIP B na Sh 25,000 kwa VIP A.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search