Tangaza nasi Tangaza nasi

September 26, 2017

DORTMUND vs REAL MADRID MIAMBA MIWILI KUKUTANA KWENYE LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA

Kuna vitu bhana hapa duniani huwa havitokei mara kwa mara na vikitokea huwa na utamu, shauku na ladha ya aina yake mbele ya macho ya mwanadamu. Mfano mmoja wapo ni kwa waislamu wanapoisubiri usiku wa laylatul kadri unaotokea mara moja kwa mwaka ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani au Chrismass kwa Wakristo inayokuja kila ifikapo Disemba. Ingekuwaje kama kila siku vitu hivi vingekuwepo? Kusingekuwa na ladha bhana!

Ndiyo maana kuna sababu nyingi kwanini binaadamu hawezi kuwa kitoweo hata kama kuna janga la njaa. Tuyaache hayo! Miamba miwili itakutana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Najiuliza hii ni burudani ya aina gani? Nani sukari na nani asali na kipi ni kitamu zaidi ya kingine? Nawaza nani ni limao na nani ni ndimu nakipi kina ladha ya uchachu zaidi ya kingine?
Timu zote zimekuwa na vikosi bora na mwanzo mzuri na hii ndiyo sababu ya kujiuliza maswali yote hayo. Pierre Emerick Aubameyang amefunga hat trick mwishoni mwa juma hili hali inayomfanya kuwa kwenye morali ya ushindi kuliko mchezaji yeyote wa Dortmund.
Muenendo wake huenda ukawa mwiba mchungu mbele ya Madrid, hivi huu mchezo hauwezi kumalizika kwa sare ya mabao 2-2? Ngoja tuone!
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka