Tangaza nasi Tangaza nasi

September 22, 2017

HIVI NDIVYO MBAO FC WALIVYOVURUGA REKODI YA SIMBA

Mbao FC imekuwa timu ya kwanza kufunga bao dhidi ya Simba tangu kuanza kwa msimu huu 2017/2018.

Simba walimudu kucheza mechi tatu bila kuruhusu bao katika nyavu zao huku kipa Aishi Manula akiwa amecheza kwa zaidi ya dakika 325 bila kufungwa.

Mbao wameibana Simba na kuilazimisha sare ya kufungana 2-2 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania bara.

Hizi ni dondoo muhimu kuhusu mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba”

Hii ni sare ya kwanza tangu Simba na Mbao zimeanza kukutana msimu uliopita katika mechi za ligi na FA Cup. Katika mechi tatu za ligi walizocheza, Simba imeshinda mbili huku mchezo mmoja wakitoka sare. Walipokutana kwenye mechi ya FA Simba walishinda.

Mbao wamefunga goli katika mechi zao zote nne za msimu (Gagera Sugar 0-1 Mbao, Singida United 2-1 Mbao, Mtibwa 2-1 Mbao, Simba 2-2 Mbao).
    Shiza Kichuya amefunga goli lake la kwanza msimu baada ya kucheza mechi tatu bila kufunga. Msimu uliopita ndio alikuwa kinara wa mabao Simba (alifunga magoli 12 kwenye mechi za ligi).
    Jamses Kotei ameweka rekoi ya kuunga bao la kwanza VPL tangu alipojiunga na Simba msimu ulipita.
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka