Tangaza nasi Tangaza nasi

December 13, 2017

CHELSEA YAIKUTA MAN U

Kwa mara ya kwanza katika historia, Willian amehusika katika mabao 3 katika mechi moja akiassist mabao ya Pedro na Bakayoko huku akifunga bao moja na kuifanya Chelsea kuibuka kidede kwa mabao 3 kwa 1.
Kwa matokeo ya hii leo Chelsea wamefikisha alama 35 sawa na Manchester United lakini Chelsea wanakuwa wamezidiwa idadi ya mabao ya kufunga huku wakiwa wametangulia mchezo mmoja.
Crystal Palace waliipiga Watford mabao mawili kwa moja, huku Julian Speron wa Crystal Palace akicheza mchezo wake wa 400 tangu ajiunge na na klabu hiyo tarehe 14/08 mwaka 2014 huku Watford wakimaliza pungufu baada ya Tom Clevery kupewa kadi nyekundu.
Stoke City ambao wiki iliyopita walizomewa na mashabiki wao kutokana na kiwango kobovu wameendelea kuboronga baada ya kufungwa bao moja kwa nunge na Burnley kwa bao lililofungwa na Ashley Barnes.
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka