banner

August 30, 2018

MASHABIKI SIMBA WAICHANA VIKALI TFF, WAISALITI STARS

MASHABIKI SIMBA WAICHANA VIKALI TFF, WAISALITI STARS

Baada ya kutangazwa wachezaji sita wa Simba kutemwa ndani ya kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, mashabiki wengi wa klabu hiyo wamoneshwa kuchukizwa na maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Jana kunako Makao Makuu ya Shirikisho hilo lililopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Stars kupitia Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, alitangaza kuwaondoa wachezaji 6 wa Simba huku akiachwa Kipa Aishi Manula pekee.

Kutokana na maamuzi hayo, asilimia kubwa ya mashabiki wengi wa Simba wamefunguka kuwa kueleza kuchukizwa zaidi na maamuzi hayo huku wakifikia hatua ya kusema hawatainga mkono Stars itakapocheza na Uganda.

Sababu za kuwaondoa wachezaji hao ni kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kwa ajili ya kuweka kambi maalum tayari kuanza maandalizi ya kucheza na Uganda.

Mbali na kutoiunga mkono Stars, mashabiki wameeleza kufuata nyayo za nyota wao, Emmanuel Okwi wakiahidi kuishabikia timu ya Uganda ambayo watacheza nayo Septemba 8 katika mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON huko Kampala Uganda.

Aidha, wengi wao wameleeza kushangazwa na maamuzi hayo ya TFF wakisema wamefeli huku wakishauri kuwa ilipaswa suala la nidhamu liende polepole.

Wachezaji wa Simba waliondolewa ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search