Tangaza nasi

December 10, 2018

VIDEO: KIBA ATAJA ALICHOTAMANI KUKIFANYA JANA DHIDI YA MBEYA CITY MKWAKWANI TANGA

Msanii wa bongo fleva ambaye pia ni mchezaji wa Coastal Union jana Desemba 9, 2018 amecheza mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara tangu asajiliwe na timu hiyo msimu huu wa 2018/19.

Kiba ametumia takribani dakika 64 akiwa sehemu ya mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na Coastal Union likiwemo lile lililosababisha kona iliyozaa goli kabla ya kufanyiwa mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Deo Anthony.

Mara baada ya mchezo huo, Kiba amezungumza na kuweka wazi hamu yake ya kufunga goli kwenye ligi kuu, akisema alitamani kwenye mchezo huu apate goli.
Pia amezungumzia sababu za yeye kuingia uwanjani na gari binafsi akidai kuwa hakuwa akiishi kambini na timu hivyo alitokea nyumbani.

Mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
JIUNGE NA Bin RUWEHY SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Michezo! Usikose kujiunga na App Yetu Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bin RUWEHY kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka