banner

October 14, 2019

KIMENUKA! PYRAMIDS WAIPELEKA YANGA CAF

KIMENUKA! PYRAMIDS WAIPELEKA YANGA CAF


Inaelezwa uongozi wa klabu ya Pyramids FC ya Misri umetuma malalamiko kwenda Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ukigomea kitendo cha Yanga kubadilisha uwanja wa kuchezea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itamenyana na Pyramids Oktoba 27 kwenye mechi ya raundi ya kwanza ambayo awali ilifahamika itanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini baadaye Yanga wakaamua ichezewe Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba.

Kufuatia mabadiliko ya uwanja huo, imekuwa kama Pyramids wameshtukia na wameamua na taarifa zinasema wametuma malalamiko hayo CAF ili kujua sababu rasmi.

Taarifa zinasema Pyramids wanaona kama ni mbinu za Yanga kuwapoteza kwenye mechi hiyo mpaka imefikia hatua ya kuhoji CAF.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi hiyo ya Play Off ambapo mshindi atafuzu mpaka hatua ya makundi ya mashindano hayo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search