banner

October 15, 2019

MZUNGU SIMBA AMUANDAA MUUAJI WA AZAM FC

MZUNGU SIMBA AMUANDAA MUUAJI WA AZAM FC


Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amesema kumuanzisha mshambuliaji wake Mbrazili, Wilker Da Silva katika mchezo wa kirafiki juzi, ni maandalizi ya nyota huyo katika kuelekea mchezo mgumu dhidi ya Azam FC.

Mbrazili huyo aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, alianza na kucheza dakika zote 90 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bandari ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo Simba ilishinda 1-0 kwa bao la Ibrahim Ajibu.

Simba na Azam zinatarajiwa kuvaana Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wilker huo ndiyo mchezo wake wa kwanza kuanza kwenye kikosi cha timu hiyo tangu ajiunge nayo. Mchezo wake wa kwanza ulikuwa ni dhidi ya timu ya vijana ya Azam ambao nao ulikuwa wa kirafiki lakini alitokea benchi.

Aussems alisema ana furaha kumuona mshambuliaji huyo akianza na kucheza dakika zote 90, licha ya kutofunga bao.

Aussems alisema kuwa amepanga kumpatia mechi nyingine mbili za kirafiki watakazocheza mkoani Kigoma dhidi ya Mashujaa FC na Aigle Noir ya nchini Burundi kabla ya kucheza na Azam.

Aliongeza kuwa mshambuliaji huyo ameshindwa kuonekana uwanjani kutokana na kusumbuliwa na majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu kabla ya juzi kumuanzisha katika kikosi cha kwanza.

“Ninafurahi kumuona akicheza vizuri, licha ya kutofunga bao.

“Kufunga bao kwake kwangu hayakuwa malengo, zaidi nilikuwa nataka kumuongezea hali ya kujiamini, pia mechi fitinesi baada ya kurejea uwanjani akitokea kwenye majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

“Nimepanga kumchezesha tena kwenye michezo miwili ya kirafiki tutakayocheza Kigoma, lengo ni kumuandaa kwa ajili ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam,” alisema Aussems.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search