banner

October 11, 2019

UONGOZI YANGA WAMGEUKA DANTE, WAMTOSA MSHAHARA

UONGOZI YANGA WAMGEUKA DANTE, WAMTOSA MSHAHARA


Uongozi wa klabu ya Yanga umeamua kukivalia junga suala la mchezaji wake, Andrew Vincent 'Dante' kuhusiana na suala lake la kugoma kuitumikiatimu hiyo kisa madai ya fedha zake.

Taarifa zinasema kuwa, kutokana na Dante kugoma Yanga hawataweza kumlipa tena fedha anazodai sababu ya kutokuwa katika eneo lake la kazi.

Mabosi wa Yanga walikuwa tayair kumlipa Dante fedha zake japo kwa mafungu ingawa mchezaji mwenyewe alitia ngumu akitaka alipwe zote kwa mkupuo.

Ofisa Uhamasisha wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, amesema licha ya mchezaji huyo kudai fedha zake hakupaswa kuendelea kukaa nyumbani badala ya kuendelea na kazi kama kawaida.

Nugaz alieleza kuwa Dante alipaswa kuendelea na kazi lakini kwa kile alichokifanya wananafirikia kutomlipa kabisa.

"Hatushindwi kumlipa fedha zake zote kama anavyotaka, lakini tuna hofu kwa sababu hadi sasa hayupo katika eneo lake la kazi na anapokea mshahara, huenda asipate mshahara wake mwezi huu sababu hayupo kazini," amesema Nugaz.



Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search