banner

January 16, 2020

ALIYEMTUNGUA MANULA NDANI YA MBAO ANA JAMBO LAKE JINGINE TENA

ALIYEMTUNGUA MANULA NDANI YA MBAO ANA JAMBO LAKE JINGINE TENA


SAID Khamis Jr mshambuliaji wa Mbao FC leo ana kazi kubwa ya kuendeleza ubabe wake aliouanza msimu wa mwaka 2018/19 uwanja wa CCM Kirumba kwa kumtungua mlinda mlango, Aish Manula bao 1-0 na kuipa pointi tatu timu yake.
Leo, Sven Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ana kibarua kizito cha kukutana na fupa hilo la Mbao ambalo lilimshinda Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji.
Akizungumza na Salh Jembe, Jr amesema kuwa maandalizi yapo vizuri kwa timu yake ni suala la muda tu kuona namna gani watapata pointi tatu mbele ya Simba.
“Tumejipanga na tupo tayari kupata matokeo, msimu huu tumekuwa na mwenendo mgumu hii inatokana na ushindani wa ligi ila tupo tayari na tutapambana kufanya vizuri,” amesema Jr.

Simba inakutana na Mbao leo Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa msimu uliopita kwa bao 1-0 jambo lililowakasirisha mashabiki na kumtupia makopo Aussems ambaye kwa sasa yupo zake nchini Ubelgiji.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search