banner

January 19, 2020

CCM KIRUMBA TENA KUWAKA MOTO LEO, ALLIANCE V SIMBA VITA YA KISASI

CCM KIRUMBA TENA KUWAKA MOTO LEO, ALLIANCE V SIMBA VITA YA KISASI



LEO Uwanja wa CCM Kirumba, Alliance FC iliyo chini ya Kocha Felix Minziro itakuwa na kazi ya kumenyana na Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu Sven Vanderbroeck raia wa Ubelgiji.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa ni wa kisasi kwa Alliance kutokana na hasira za kupoteza mechi zake zote mbili ilizocheza na Simba ilipopanda daraja msimu wa 2018/19.
Mechi iliyowakutanisha Uwanja wa CCM Kirumba, Alliance ilikubali kuchapwa mabao 2-0 na ina kumbukumbu ya kufungwa mabao 5-1 ilipocheza na Simba Uwanja wa Taifa hivyo ina mzigo wa kufungwa jumla ya mabao 7-1 jambo ambalo linawaumiza viongozi wa Alliance pamoja na wachezaji.
Simba hesabu zao ni kubeba pointi sita za kanda ya ziwa baada ya kutoka kushinda mbele ya Mbao FC mabao 2-1 leo watakuwa wanazipigania pointi za Alliance ili kuondoka na pointi sita za kanda ya ziwa msimu huu huku Alliance wakizipigia pointi tatu za Simba kujiongezea hali ya kujiamini na nafasi ya kubaki ndani ya ligi.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wamecheza jumla ya mechi 15, wametoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja mbele ya Mwadui FC huku wakishinda mechi 12 na pointi zao 38 huku Alliance ikiwa nafasi ya 13 imecheza mechi 16 imeshinda mechi tano, sare tano na imepoteza mechi sita ikiwa na pointi 20 kibindoni.
Kocha wa Alliance, Minziro amesema kuwa anawaheshimu Simba ila hana mashaka na uwezo wa vijana wake kutokana na spidi wanayomuonesha mazoezini ana imani watapata pointi tatu na Sven wa Simba alisema kuwa wanahitaji pointi tatu na wachezaji wake wapo vizuri.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search