banner

January 14, 2020

KUMBE! SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2 INAWAUMIZA YANGA, MILIONI 150 ZILIZOYEYUKA ZINAWAUMA KINOMA

KUMBE! SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2 INAWAUMIZA YANGA, MILIONI 150 ZILIZOYEYUKA ZINAWAUMA KINOMA


IMEELEZWA kuwa sare ya mabao 2-2 waliyoipata Yanga inawaumiza kutokana na kupoteza mkwanja mrefu ambao ulikuwa mezani.

Januari 4,2020 Yanga ilikaribishwa na Simba kwenye mchezo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara na walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ambao bado unawaumiza mashabiki wa Simba ambao wengi walikuwa wakimlaumu mlinda mlango Aishi Manula kwa kufungwa bao la kwanza nje ya 18 na Mapinduzi Balama inaelezwa kuwa imewaingizia hasara Yanga ya shilingi milioni 150.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa kabla ya mechi, viongozi na wadhamini wa timu hiyo GSM waliweka mezani dau la shilingi miloni mia mbili endapo Yanga ingeifunga Simba kwa idadi yoyote ya mabao.

"Kabla ya mechi mabosi waliweka mezani milioni mia mbili ambazo timu ingeshinda basi zilikuwa ni halali yao kuzitumia. Tofauti na mechi nyingine bonasi ilikuwa ni milioni kumi sasa uzito na ukubwa wa mechi yetu dhidi ya Simba basi dau likapanda.

"Baada ya mechi ile mchezaji bora ambaye alikuwa ni Balama Mapinduzi alikabidhiwa godoro ila wachezaji walipewa milioni 50 kwa kuwa walipambana na walipata ile sare ya kufungana.

"Sare ya kufungana mabao 2-2 licha ya kwamba mechi imechezwa siku nyingi bado ni kidonda kwetu yaani hasara ya milioni 150 inauma ujue, basi wana bahati walianza kujilinda baada ya kurudisha mabao 2 ndani ya dakika saba," kilieleza chanzo hicho.

Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti na Deo Kanda alifunga moja na yale yaYanga yalifungwa na Mapinduzi Balama na Mohamed Baka.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search