banner

January 15, 2020

MANARA AZIDI KUUMIWA NA MTIBWA SUGAR, AFUNGUKA MENGINE MAZITO KUHUSIANA NA SIMBA

MANARA AZIDI KUUMIWA NA MTIBWA SUGAR, AFUNGUKA MENGINE MAZITO KUHUSIANA NA SIMBA


Wanasimba wenzangu!!

Najua maumivu mliyopitia jana na nnafahamu karaha mnazopata toka kwa watani zetu, lakini niwaambie kitu kimoja, hili kwetu ni funzo, ni funzo kwa kila mmoja klabuni.

Viongozi,Benchi la ufundi na hata wachezaji wetu.

Wanasimba wa leo hawapo tayari kufungwa na hasa kama unafungwa kirahisihisi.

Kocha wetu atakuwa kaelewa nn mnataka wenye timu na wachezaji bila shaka watapambana ili kuwapa Wanasimba mnachostahili
Mm imani yangu ni kubwa sana kwao, hakuna shaka yaliyotokea jana ni historia isiyofaa kurejewa.

Sote tunaumia lakini hii ndio Raha na karaha za football, mtu wa mpira lazma upitie tamu na chungu za kushabikia soka.

Now akili yetu tuelekeze Mwanza ktk mechi mbili ngumu zijazo.

Tushirikiane kupata points sita za CCM kirumba
Insha'Allah tutafanikiwa 🙏


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search